Mchezaji wa zamani wa Yanga, Abdallah Yassin ambaye alikuwa akichezea timu ya Fanja ya nchini Dubai, anatarajia kuondoka kesho kutwa kuelekea Norway kwaajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Akizungumza
jana jijini hapa, Abdallah alisema kuwa, anakwenda Norway kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
“Nimeondoka
Yanga miaka miwili iliyopita, nikaenda Dubai nilipocheza soka la
kulipwa kwa miaka miwili na sasa meneja wangu ambaye ni kaka yangu
Ostadhi Juma na Musoma, ameniambia tukutane Dar es Salaam kwaajili ya
kwenda Norway kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa” alisema
Abdallah.
“Nakwenda
kufanya majaribio Norway si kwamba Dubai walikuwa hawanilipi vizuri,
hapana ila natafuta maslahi mazuri zaidi na huduma nzuri zaidi kwani
umri unakwenda na ndoto lazima zitimie kupitia
soka”alisisitiza.
Na
kuongeza kuwa, aliondoka Yanga kwasababu hakuwa akilipwa mshahara ila
alikuwa akipewa posho, Fanja alikuwa akilipwa mshahara mzuri ila hawezi
kuwasahau viongozi Ayub Nyenzi na Lucas Kisasa waliomsomesha katika
Sekondari ya Makongo na baadaye kuichezea Yanga.
Huku
akiamini siku moja atakuja kuitumikian timu ya taifa “Taifa stars”
kwani anapenda sana kuichezea timu hiyo, licha ya kutowahi kupata nafasi
katika kikosi hicho.
“Nilikuwa
na ndoto za kwenda Ulaya miaka mingi na nilishawahi kupata nafasi ila
kutokana na uloho wa baadhi ya viongozi ndoto hazikutimia, wakati huo
tukiwa Makongo chini ya kocha marehemu James Kiiza”aliongeza.
“Tuliwahi
kuhitajika na wachezaji wa zamani wa Liverpool Less Ferdinand na John
Banzi ili kucheza Ulaya lakini walipokuja walikuta hali si sawa na
makubaliano waliyowekeana na viongozi Jack Pemba na Idd Kipingu; kwa
madai kuwa walitoa fedha nyingi ili tupate matunzo mazuri mimi na Jerry
Tegete, Nelson Kimati, Mustapha Mabrouk na Kigi
Makasy”anasema Abdallah.
No comments:
Post a Comment