Tuesday, December 3, 2013

MAHABAAT


FAHAMU MAMBO 4 MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!!!! SOMA ZAIDI HAPA..... ONYO! STORI HII NI KWA WENYE MIAKA (18+) TU



Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia.
Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana!


Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa.
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.
Kuoga pamoja

Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.
Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.
Kusifiana

Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.
Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.
Kuelekezana

Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika.
Zungumzieni maisha

Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.
Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu.

MAHABAAT


HIVI KUMBE KUHIFADHI UPENDO WAKO KWA MWANAUME AMA MWANAMKE PASIPO MAPENZI YA DHATI NI BALAA?!!!.


DU!


NI siku nyingine tunakutana katika ukurasa wetu wa kupeana mambo muhimu ya kuboresha uhusiano wetu na wapenzi wetu. Nawashukuru wasomaji wetu wote ambao wamekuwa wakinipa moyo kwa kunitumia ujumbe mfupi wa maneno na wengine kunipigia moja kwa moja ! 

Baada ya utangulizi huo, sasa tugeukie katika mada yetu la leo.

Hebu jiulize; mpenzi wako anapokuambia anakupenda, inatosha kweli kukuthibitishia kuwa anakupenda kwa dhati na uendelee kumwamini? Hapa kila mmoja anaweza kuwa na jibu lake lakini kwa wataalamu wa Saikolojia ya Mapenzi hawakubaliani na hoja hii.

Kwa nini? Kwa sababu neno nakupenda ni jepesi sana katika hali ya kawaida kutamkika lakini lina maana kubwa sana linapokuja katika ulimwengu wa mapenzi ya dhati.

Naam! Ulimwengu wa mapenzi ya dhati kwa sababu kuna wengine hawana mapenzi ya kweli wanapotamka neno hili. Wanasaikolojia wa masuala ya uhusiano wanaeleza kwamba neno hilo linaweza kuwa na maana ikiwa litalandana na matendo.

Wengi wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu katika uhusiano. Wapenzi wao wamekuwa hawaeleweki kama wana mapenzi ya kweli au la, kutokana na mambo wanayowafanyia lakini wakati huo huo neno nakupenda limekuwa halikauki midomoni mwao.

Ni haki yao kuchanganyikiwa lakini kuchanganyikiwa huko kunatokana na kutokujua mambo ya uhusiano vyema. Mpenzi msomaji wangu, inawezekana wewe ukawa mmoja wa watu hao, hii ni nafasi yako mahususi kwa ajili ya kumfahamu mpenzi wako vyema.

Kwa nini uhifadhi moyo wako kwa mpenzi asiye na mapenzi ya kweli? Je, utajuaje kama mwenzi uliyenaye ana penzi la dhati moyoni mwake? Hebu tuone vipengele vifuatavyo; 

ANAKUPUUZA...
Hili ni tatizo kubwa katika uhusiano na hasa kwa wasichana. Wanaume wengi wa siku hizi ambao wana mapenzi ya ubabaishaji huwapuuza wenzi wao. 

Hivi utawezaje kukubali kuendelea kuitwa mpenzi na kila wakati mtu huyo anakuambia anakupenda lakini anakupuuza? Bado utaendelea kumhesabia mtu huyo anakupenda? Kwa lipi hasa wakati hazingatii yale unayomwambia hata kama yana msingi kiasi gani katika maisha yenu yajayo ? 

Mpenzi mwenye mapenzi ya kweli, kwanza huzingatia mawazo ya mpenzi wake, hupima kila aambiwalo na kulifanyia kazi. Huwezi kumpuuza mtu ambaye unampenda hata siku moja. Hiki ni kipimo cha kuzingatia wakati wa kutafuta mpenzi wa kweli. 

Hata kama anakuambia anakupenda mara ngapi kwa siku, lakini kama haoneshi kuthamini umuambiayo, penzi la mtu wa aina hii lina mushkeli. 

Anayekupenda huwa makini kukusikiliza kwa kila kitu. Mwingine anaweza akawa anamshauri vizuri sana juu ya maisha lakini mwanaume huyo akawa hana ‘time’ kabisa naye. 

Usingoje kujidhalilisha zaidi ya hapo, huyu atakuwa hakupendi ila ana vitu anavyovipata kwako ndiyo maana anajilazimisha kukuambia ‘nakupenda’ ya kinafiki ili aendelee kupata anachokipata kutoka kwako. Upo hapo ?. 

ANAHOFIA SIMU YAKE.
Hapa kuna utata mkubwa! Wengi hujitetea kuwa simu ya mkononi ni kwa ajili ya mhusika na siyo vinginevyo. Hapa kuna ukweli fulani lakini wengi walio katika uhusiano hutumia kijisababu hiki kama nguzo ya kuendelea kufanya mambo yao yasiyofaa kwa kutumia simu zao. 

Hata hivyo, wanasaikolojia ya mapenzi wanaunga mkono hoja hiyo, maana wakati mwingine unaweza ukachukua simu ya mpenzi wako, ikasababisha mgogoro mkubwa. 

Pamoja na hilo, kumgundua mwizi ni rahisi sana, ukikutana naye hata kama humfahamu unaweza ukajikuta unamhisi, ndivyo ilivyo katika uaminifu wa simu za mikononi. Ukiona umeshika tu simu yake anakuwa mkali, jua kuna kitu kinaendelea. 

Simu inapigwa halafu ghafla anatoka kwenda kupokelea nje, jiulize mara mbili. Lakini wakati mwingine ukiona simu yake inaita halafu jina linalotokeza kwenye simu yake lina utata, anza kufikiria mara mbili. 

Kwa mfano uliona jina limeandikwa: G45, BM, Chizi, Magomeni, Jumapili na majina mengine yenye utata au yaliyofupishwa, jua kuna mambo yanaendelea chini ya kapeti !.

Ukianza kuhisi tofauti kidogo juu ya simu yake, anza kumchunguza na mara nyingi akigundua unamchunguza kuliko umharibie mambo yake atakuwa tayari kuachana na wewe. Kukuambia anakupenda pekee hakutoshi kwa kasoro hii. 

HATAKI KUKUTAMBULISHA!
Kukupenda kwake hakuwezi kukamilika ikiwa hataki kukutambulisha. 


Ni kweli kwamba jambo hili siyo la haraka lakini unaweza kukuta wapenzi wapo katika uhusiano kwa mwaka mzima au zaidi lakini hakuna ndugu yeyote wa upande wa mwanaume anayemfahamu! Ukiachilia mbali ndugu lakini hata rafiki zake wa karibu hawamfahamu, hilo ni tatizo. 

Kwa hali kama hiyo hata kama jamaa atakuwa akirudia kusema anakupenda mara ngapi, ana mapenzi ya kweli? Hakika hakuna. 
Dada zangu wapendwa, wanaume wamejaliwa sana ujuzi wa kuongea, ndimi zao ni tamu zisizokaukiwa na maneno lakini hayo huyazungumza wakiwa na malengo na mipango yao ambayo inaweza kufanikiwa akiwa na wewe. 

Kwa misingi hiyo atashindwaje kukuambia anakupenda hata kama ni mara mia tisa tisini? Siyo kazi kusema nakupenda kutoka mdomoni lakini inapokuja maana ya neno hilo kutoka moyoni ndiyo shughuli inapoanzia. 

Kwa leo naweka kituo kikubwa hapa, wiki ijayo usikose katika sehemu ya mwisho ya mada hii ya kusisimua.

Monday, November 11, 2013

MAKALA


Maji moto ya Mutagata kugharimu mil.22 kuweza kutoa huduma bora, Kagera

Jumla ya shilingi za kitanzania milioni 22, 935, 250 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kulala wageni na vyoo kwa wagonjwa na watalii wanaokwenda katika msitu wa hifadhi ya majimoto katika kijiji cha Rwabigaga wilayani Kyerwa mkoani kagera.
Msitu wa Hifadhi ya Maji Moto (Mutagata Hot Spring catchment forest) ni moja ya kivutio kikubwa katika wilaya ya Kyerwa, unaopatikana katika kijiji cha Rwabigaga eneo la Mutagata, kata ya Kamuli, tarafa ya Kituntu/Mabira.
Akizungumzia ujenzi huo, mwenyekiti wa kijiji cha Rwabigaga Froni Nestory alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya kubaini kuwa na uharibifu wa mazingira lakini pia utasaidia katika kuongeza pato la serikali ya kijiji hicho.
“Tumeamua kujenga nyumba ya vyumba vinne na vyoo vyenye mashimo mawili ili wageni kutoka nje ya kata ya Kamuli watakapohitaji huduma hapa watalipia shilingi 5,000 kwa kila mmoja kwa lengo la kukuza pato la kijiji pia na gharama za utunzaji wa eneo hili la kihistoria,” alisema.
“Ujenzi huu ni nguvu za wananchi ambao kila mmoja alichangia shilingi 2,000 huku shirika la Hifadhi Mazingira Yakutunze (HIMAYA) ambao walichangia kiasi cha shilingi 935,250 kwaajili ya ujenzi wa vyoo ili kuepuka hadha ya kujisaidia hovyo hasa msimu wa mvua, serikali ya kijiji ikichangia kiwanja na shilingi za kitanzania milioni 22 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya kulala wageni,” alisisitiza Nestory.
Aliongeza kuwa, “baada ya ujenzi huo kukamilika tuta tangaza tenda ya kulisha chakula eneo hili; hadi sasa hatujapata msaada wowote kutoka Halmashauri licha ya viongozi mbalimbali kuhudhuria wakiwemo wakuu wanne kupanda miti ya asili eneo hili na pia kupelekea mapendekezo yetu katika ngazi ya wilaya lakini hakuna jibu lolote hadi sasa”.
Msitu huo ni umbali wa kilomita 70 kutoka makao makuu ya wilaya; Msitu huu ni wa kijani kibichi muda wote uliotanda miti ya Misambya (Markhamia Lutea) na miti mingine ambayo majina yake hayafahamiki vyema.
Katika msitu huu vipo vyanzo vinne vya maji moto, vyanzo hivi ni; Kasiyoza ambacho ni chanzo kikubwa cha maji moto katika eneo hili ambalo maji yake ni nyuzi joto 60-90; Chabakazi ambalo ni eneo dogo linalotoa maji ya moto yenye nyuzi joto 40-60; Katagata kake hili ni eneo jingine ambalo maji yake ya moto yana nyuzi joto 30-50 na Chandagala chenye maji ya baridi.
Katika kutafuta ushuhuda wa tiba hii inayoaminika kwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita kuwa inatibu na wagonjwa kadhaa kuthibitishwa kupona, nilikutana na mama mmoja aliyekuwepo eneo hilo kwa matibabu.
“Nashukuru sana kuletwa hapa maana nimeugua hii miguu kwa miaka sita bila kutembea leo hii kama unavyoniona naendelea vizuri kwani naweza kutembea, na nina siku tatu toka nimefika hapa,” alisema Kotilda Marco (35) ambaye alikuwa amepelekwa eneo hilo kwa ajili ya kupata tiba ya miguu,” Bi Kotilda alieleza.
“Maji haya ni tiba yenye kuponya kwani leo unaniona hivi ila nimeletwa hapa sikuwa naweza kutembea hata kwenda kujisaidia nilikuwa napelekwa, lakini sasa naweza kwenda hata pale juu kuoga mwenyewe na kurudi ama kweli Mutagata ni ponyo kwetu,” aliongeza mama huyo.
“Historia inaonyesha kwamba chem chem hii ilitumiwa na machifu kuoga; Chifu Rumanyika alitembelea eneo hili na kuliwekea Baraka, akaitukuza chem chem hii na kulitangaza eneo hili kuwa sehemu takatifu na kuanzia wakati huo, maji hayo hutumika kwa ajili ya tiba ya magonjwa ya ngozi kama vile upele na mapunye, kifua, uvimbe wa miguu, magoti n.k.
”
Boniface Mshonga ambaye  ni Mwenyekiti  mstaafu wa kijiji cha Mutagata.
“ Licha ya chanzo hiki kusaidia katika kuponya lakini ni moja ya utalii ambao kama serikali itaweza kukitumia vyema; ila inavyoonekana chanzo hiki kinaweza kuharibiwa na wakazi wa eneo hili ambao wamekuwa wakiyatumia maji haya kwa kufulia na kunyweshea mifugo huku misitu hii wakitumia katika matumizi ya nyumbani,” alisisitiza.
Hata hivyo, ili kupata historia zaidi nilimtafuta mzee maarufu mwenye umri mkubwa ili kuweza kunijuza hasa kuhusu chanzo cha maji haya.
“Aliyeleta maji haya ni shangazi kutoka katika utemi katika kabila la Buganda, wakati alipokuwa akitokea Rwanda kuelekea Uganda na alipofika hapa alikuwa amevimba miguu na amechoka sana yeye pamoja na watumishi wake ndipo alitamka kuwa ee Mungu ungenisaidia maji ya kukanda hii miguu ili niweze kuendelea na safari na kasha maji hayo yakatokea na kuyabariki kuendelea kutumika hadi leo,” alisema mzee Busisi kayombagani (101) ambaye ni mzaliwa wa eneo hilo.
“Baada ya kuyaacha maji hayo kwa kuendelea na safari ndipo yalibaki yakiangaliwa na kabila la Wahinda chini ya mtemi(chief) Rumanyika hadi ukoo huo ulivyoamua kuhama eneo hilo na mmiliki kufariki, eneo hilo likamilikiwa na kabila la ukoo wa Muhunga ambao walikuwa wakimuita mtemi Rumanyika babu kutokana na kuozana hadi leo,” alisisitiza.
Na kuongeza kuwa,“kwasasa mila na desturi za eneo hilo zimebadilika kwani zamani hakuruhusiwa mwanamke ambaye yupo kwenye hedhi wala mtoto ambaye hajaota meno wala kutenda tendo la ndoa eneo hilo na alipokuwa akikosea mmoja wapo lazima madhara yatokee wakati ule ule, lakini leo unaona watu wanaoga katika maji hayo na watoto pia wanaoga hadi mifugo inanyweshwa hapo na hii yote ni kutokana na watu wa kabila linalomiliki kushindwa kufanya matambiko ambayo yalifanywa hapo awali kama vile kuchinja, ng’ombe na kunywea katika eneo maaalum pombe ya kienyeji”.
Tunapozungumzia historia ya watu wa mahali fulani hatuna budi kuzungumzia Jiografia ya sehemu husika, hali ya hewa na mazingira, wakazi wake, uoto wa asili, utamaduni wao, utawala, mawasialiano na uchumi.
Lengo la kutafuta na kuifahamu vyema historia ya watu wa Kyerwa ni la msingi sana kwa kuandaa mazingira ya watu mbalimbali  ili waweze kuielewa vyema  historia ya Kyerwa, kukusanya na kuzihifadhi zana na kumbukumbu za kimila na jadi ambazo katika siku za karibuni zinaelekea kuanza  kupotea.
Makala hii inachambua kwa kina historia ya msitu wa hifadhi ya maji moto ambao kwa asili unapatikana Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera.
Kwa upande wake mtunza eneo hili ambaye anadaiwa kutoka katika ukoo wa Muhunga ambapo mtemi Rumanyika alioa huko, hakusita kuelezea kile anacho kifahamu katika eneo hilo.
“Kama unavyofahamu mtemi Rumanyika alifanya mambo mengi ambayo hadi leo yamebaki ni historia isiyopotea, hivyo katika kumuenzi ndio maana unaona eneo hili linaendelea kuwepo na vitu vyake vya asili ambavyo nitakwenda kukuonyesha,” alisema Angelo Mathias mtunza eneo hilo.
“Kama unavyoona jiwe hili la kukalia ndipo alipokaa Kanyabugondo shangazi wa utemi wa Buganda na mpaka leo hutumika kukalia na kuogea kwa wagonjwa wanaofika eneo hili na hapa pembeni sehemu ya kuweka sabuni au marashi kwani machifu walitumia kuwekea sabuni wakati wa kuoga na palitengenezwa kwa mikono na malkia huyo; pia hili bao lilitengenezwa kwa mikono, na chifu Rumanyika na wageni wake walitumia wakati wa kupumziko lakini eneo hili lilitumika wakati wa tambiko na hapa ni eneo la kutupa mawe au pesa kwa wanaofika kupata huduma hapa,” aliongeza.
Mbali na kivuto hicho cha maji moto pia katika wilaya ya Kyerwa na Karagwe kuna mapori manne ya Akiba za wanyamapori ambayo ni Rumanyika Orugundu, Kimisi, Ibanda na Burigi.
Mbuga hizi zina wanyama wengi kama vile pofu, nyemera, mamba, viboko, twiga, simba, kuro, nyati, tembo na ndege wa aina mbalimbali.
Mapori haya ya Akiba mbali na kuwa kivutio kwa watalii na wananchi wanaopenda kuangalia wanyamapori, mito na mabonde;  vile vile hutumika kwa shughuli za uwindaji wa kitalii. 

Wanyambo ambao ndio wenyeji wa eneo hili ni kabila lilokuwa miongoni mwa makabila makubwa na yenye nguvu za kivita na kiuchumi.

Utawala wa kabila hili ulikuwa wa kifalme ulioongozwa na wafalme “Abakama” 14 kwa nyakati tofauti huku watu wake ni wakulima na wafugaji.

Kabila la Wanyambo linapatikana katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera.

Inaaminika kuwa asili ya jina la kabila hili ni eneo la Maziwa Makuu na jina la kabila hilo limetokana na aina moja wapo ya ndizi inayofahamika kwa jina la Enyambo.

Aidha neno nyambo linamaanisha mtu au kitu au mmea asilia pia yupo ng’ombe wa asili wilayani Karagwe ambaye anajulikana kwa jina la Enyambo linalofahamika katika nchi za Uganda na Rwanda.

Himaya ya mfalme wa Karagwe ilikuwa ndiyo utawala mkubwa katika maeneo ya maziwa makuu kwa miaka kama 500 na Bweranyange Mji Mkuu wa Mfalme wa Karagwe ndipo alikaa mfalme Ruhinda wa kwanza, mwanzilishi wa himaya za Kihinda.

Ruhinda alitawala eneo lote la Karagwe, Ankole, Kihanja, Ihangiro Biharamulo Bushubi, Bugufi Kaskazini, kipakana na Bunyoro na mto Mwiruzi Kusini ya Biharamulo na Mkoa wa Kigoma.

Licha ya kutofahamika katika Tanzania ya leo sambamba na kupanda na kushuka kwa umaarufu wa kabila hilo.

Himaya ya mfalme wa Karagwe hiyo ilitukuka na kuandikwa kwenye magazeti ya ulimwengu wakati wa wavumbuzi hususani Uingereza zaidi ya miaka 1600.
Jina “ Karagwe “ ambalo limezaa wilaya mpya ya Kyerwa kutokana na simulizi za wazee wetu mbali mbali na watafiti wa historia ya Karagwe kama (Katoke 1975;162) inaelezwa kwamba  jina hili linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya  ya Karagwe, kwenye kijiji cha Kandegesho, kata ya Nyakakika ambacho mtawala (Omukama) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza.
Na kwamba kumbukumbu hii ya “Karagwe ka Nono “inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia wa Karagwe kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara.
Inasemekana kwamba Nono son of Marija alikabidhi madaraka yake bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote kwa ajili ya kuokoa watu wake waliokuwa wanakabiliwa na wimbi la njaa.
Birigitta Farelius 2008 katika utafiti wake anasema “ Popote unapokuta ng’ombe machungani katika Afrika ya Mashariki macho huvutiwa sana na ndege weupe (white cow herons) wajulikanao kama Nyange Nyange , nao watu wa Karagwe huwaita Enyange, wakifuatana na ng’ombe huku kazi yao kubwa husaidia kudonoa kupe na wadudu wanashambulia mifugo.
Makao makuu ya Omukama Rumanyika wa Karagwe yalikuwa katikati ya makundi ya wafugaji na kulikuwepo na ndege hawa wengi  na hivyo kupewa jina la Bweranyange kutokana na ndege hawa kupenda kutanda eneo hili muda wote
Na hili linathibitishwa na simulizi za wenyeji wa eneo hili ambao wengi walikuwa wafugaji, na sisi pia tunalazimka kukubaliana na matokeo ya utafiti huu unaonyesha chimbuko la jina la Bweranyange wakiwa na maana sehemu safi na nyeupe (makao makuu ya mtawala wao) kutokana na umaarufu wa ndege hawa.


Ni kutokana na ukweli huu wenyeji walitunga wimbo maarufu wa kumsifia mtawala wao, na kwa mtawala halisi na makini kama alivyokuwa Omukama Rumanyika alitakiwa kuwa na roho nyeupe ya upendo kwa watu wake na wimbo huu ulikuwa unaimbwa popote pale alipotembelea na kulala.
Wimbo huu uliwaasa na kuwaonya wananchi kuwa wasikivu, wastaarabu, wenye kufuata kanuni, sheria na kutokuwa wasumbufu kwa mgeni wao aliyewatembelea.

“Mtayomba mwalirwa enyange ……….
Mtayomba …………………………….
Ne enyange ti nyange …………………
N’omwana ‘womuntu ……………..
Mtayomba …………………………..
Leba no omwana wo omuntu ……….

Mtayomba ………………………….” Hii ni sehemu ya wimbo huo.
Taarifa za Utafiti huu unashabihiana kwa karibu sana na ule wa Bwana HALLEY katika kitabu chake cha “An African Survey “ ukurasa 23/24 “ akielezea kwamba kaskazini magharibi mwa ziwa Victoria ‘’ Watu wa makabila ya Waganda, Wanyankole, Watoro, Wanyoro na makabila manane ya wilaya ya Bukoba katika Tanganyika na Ruanda (Nchi ya udhamini ya ubeligiji) ni mchanganyiko wa makabila ya wenyeji wakulima wabantu na makabila ya wafugaji wa kihima toka kaskazini ambao yanasadikiwa kwamba yalizishambulia nchi hizo zama za miaka mia tatu iliyopita na kuwashinda wenyeji wake.
KUHUSU BIASHARA
Mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwa karne ya 19, habari za kushamili
kwa Karagwe kutokana na biashara zilikuwa zimesambaa sehemu mbalimbali  za nchi ya Tanganyika pamoja na nchi za jirani za Rwanda, Kongo, Uganda, Burundi na hata nchi za Falme za Kiarabu.
Wakati huo Karagwe ilikuwa imekwisha tembelewa na wajasiliamali toka Unyamwezini na Usumbwa ambao walileta chumvi toka Uvinza na chuma toka Katanga (nchini Kongo). 


Hili linathibitishwa na msemo wa kinyambo wa muda mrefu unaosema “Omwonyo ngunula, chonka Omushumbwa nanunka”kwa kiswahili maana yake ni kwamba chumvi yao ni tamu pamoja na kwamba wachuuzi wenyewe wanatoa harufu mbaya ya jasho kutokana na safari yao ndefu.



Inaaminika pia kwamba Wanyamwezi walifika Karagwe wakiwa watu wa kwanza kufanya biashara na kwamba walileta chumvi, visu, pilipili, na matunda kama vile  maembe, machungwa na mtama kabla ya Waarabu kuingia ambao walijenga Kituo chao maeneo ya  Kafuro na Kitengule.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa wakati Omukama Rumanyika Orushongo anaingia madarakani, Karagwe ilikuwa tayari imekua kiuchumi kiasi ambacho wafanyabishara toka maeneo ya mbali walikuwa wameanza kuingia Karagwe wakifanya biashara ya meno ya tembo, mazao ya chuma (Iron products)kama vile visu, majembe na vitu vingine wakibadilishana na bidhaa waliyoleta toka maeneo waliyotoka.
Shughuli za Kisiasa, biashara na watu wa mbali (Tabora na Pwani) ilianzisha na kujenga mahusiano mazuri na watawala (Abakama) wa Karagwe, kiasi kwamba Omukama Rumanyika I wakati huo alilazimika kumteua msadidizi wake (Kiyango kya Mpiga Ifumula Bikungu) kuwa Balozi wake katika tawala za jirani zake ambaye wakati huo alikuwa akisafiri kati ya Bweranyange, Buganda, Bunyoro na Tabora.
Kazi kubwa ya mteule Kiyango kya Mpiga Ifumula Bikungu ambaye unaweza kumuita Kama balozi ilikuwa ni kufanya mawasiliano na kuimarisha kati ya Mtemi Rumanyika na watawala wa sehemu hizo. 
Balozi huyu alionekana kupata sifa nyingi za utendaji kazi, sifa ambayo ilitolewa wazi wazi na wageni kama Captain John Hanings Speke na Grant (katika kitabu chake kiitwacho “The jouney of discovery of River Nile” ) walipozuru Karagwe, ilikuwa ni kupitia kwake wageni hawa waliweza kupokelewa na watawala ikiwa ni pamoja na Omukama Rumanyika bila matatizo yeyote. 


Haya yanathibitishwa na mzee wetu marehemu Profesor Katoke (1975;55) ambaye aliandika
“Ikumbukwe kuwa Speke na Grant walipata upinzani mkubwa katika sehemu zingine za Kigoma na Tabora ambapo waliingia bila kuwasiliana na Kiyango, waliweza kuzuiliwa kwa muda na wakati mwingine kutozwa ushuru mkubwa na watawala wa maeneo hayo wakiwa safarini   kuelekea Karagwe”, hii inathibitisha umuhimu wa Balozi huyo Kiyango cha Mpiga Rufumura Bikungu.

Karagwe ilitumika kama njia pekee ya kufikia utawala wa Buganda kwa wageni toka Pwani na Zanzibar.

Kati ya Novemba 1861 na Februari 1862 John Hannington Speke na James Grant walikaa miezi mitatu Kafuro jirani na Bweranyange na wakaandika kwa kirefu juu ya mila na desturi za Karagwe chini ya mfalme Rumanyika Orugundu Rzinga Mchuchu wa Nkwanzi ambalo ni jina la utani lenye maana ya shujaa mfuga nywele ndefu mwana wa Nkwanzi.

Na kwamba, kwa hivi sasa kuna hifadhi ya wanyama ya rumanyika Orugundu kuenzi mtawala huyo ambayo kwa mashariki yake katika kijiji cha Ibamba kunapatikana mto wenye maji moto ya Mutagata”anasema Tuluhungwa.

Historia ya kabila hili ilifahamika ukanda wote wa Ziwa Victoria Magharibi pamoja na nchi za Rwanda na Burundi Kutokana na uhunzi wa mapambo mengi ya kifalme yalitengenezwa na kuhifadhiwa kwenye ngome ya mfalme.

Mapambo hayo yalipendwa na mengine yalichukuliwa na Wajerumani, walipewa zawadi na Omukama Rumanyika.

Ni kabila lililoheshimika na wanyambo walijivunia Unyambo wao hali iliyoibua misemo kama, Ndyu Munyambo akala nakalenje, Omunyambo agamba echabweine.

Kabila la wanyambo ni miongoni mwa makabila makubwa Mkoani Kagera mengine ni Wanyambo wenyewe, wasubi, washubi, wahangaza, wazinga na wahaya.

KUPOTEZA UTAJIRI
Karagwe ilianza kupoteza utajiri wake katika miaka ya 1880 na 1890 ambapo wakoloni wa kijerumani walikuwa wakishidana kuligawana bara la Afrika huko Berlin 1884 na baadaye wakati Zanzibar na Buganda zilikuwa tawala zinazolindwa na mfamle wa Uingereza.

Karagwe iliangukiwa na nuksi ambazo zilifika tawala nyingine zote kubwa katika historia kama za Alexander mkubwa utawala wa Kirumi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vimeanza wakati Speke na Grant wakiwa Karagwe Novemba 1861 mpaka Desemba 1862 Matokeo yake ilikuwa kupungua kwa amani na kuihama Karagwe upande ulioshindwa na kupunguza wingi wa watu.

Pili ugunduzi wa njia fupi toka Mombasa kwenda Uganda kulitoa Karagwe kwenye njia Kuu ya biashara ya kimataifa na kupunguza umaarufu wake. 

Magonjwa ya mifugo kama ng’ombe sotoka ilishambulia mifugo ya wakazi wa karagwe katika kipindi hiki na kupunguza utajiri wa Karagwe pia wakoloni walikuwa hawavutiwi na nchi maskini.

Karagwe iliathirika kisiasa na kiutawala baada ya wafalme wake wengi kufa wakiwa wadogo bila kuacha warithi walioishafikia umri wa kutawala, ikalazimu kutawala kwa kutumia viongozi wa muda kama vile Kakoko waliotawala kwa ukatili na kuharibu himaya.


Pia Karagwe haikupewa kipaumbele katika mipango ya wakoloni wa Kijerumani kulifanya Wamisionari kutovutiwa kuweka vituo vyao Karagwe.

Wamisionari wa Kikatoliki walianzisha vituo vyao Kashozi 1892, Bunena 1905, Kagondo na Rubya 1904, Katoke Biharamulo na kuanzisha shule sehemu zote hizo.

Misheni ya kwanza Karagwe ilianzishwa 1934 baada ya miaka 40 baada ya kumpata Padri wa kwanza mwafrika wa kwanza Oscar aliyepadrishwa Bukoba 1917 ambaye wa kwanza Karagwe Padri Rwakiboine alipandrishwa 1943 miaka 26 baadaye na shule na hospitali zilifata misheni.

Kwasasa Karagwe na Kyerwa imekumbwa na tatizo la kukosekana kwa mvua hali inayopelekea mazao mengi kukauka, hivyo wakazi hao kukumbuka utawala wa kichifu ambao haukuwahi kuonekana kwa tatizo hili la kukosekana mvua hadi sasa.

Thursday, November 7, 2013

MAVAZI


Mavazi kwa mwanadamu ni suala lenye umuhimu mkubwa lakini kwa mwanamke lina umuhimu wa kipekee siyo tu ili kuboresha mwonekano wa mhusika, bali pia kueleza haiba yake.
Ni wazi kuwa itakuwa kazi rahisi kumwelezea mwanamke husika alivyo kwa kumtazama namna anavyovaa, hivyo unaopaswa kuelewa ni kwamba mitindo ina nafasi kubwa katika kueleza tabia na mwenendo wa kila siku wa mtu .
Katika hilo wanawake wanatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kujipamba na wakati mwingine husifiwa kwa kuwavutia wengine kuwa watanashati.
Pamoja na sifa hiyo wanawake hufanya makosa mbalimbali katika uvaaji. Hii mara nyingi hutokana na uelewa mdogo katika suala zima la uvaaji.
Je, unapenda kufahamu dondoo mbalimbali za uvaaji? Soma hapa:
1. Unapojaribisha nguo, hakikisha umesimama wima pia jiweke katika pozi tofauti. Kwa kufanya hivyo utaweza kugundua urefu wako, pia utajionea unavyovutia katika vazi husika.
2.Elewa umbo lako linavyovutia. Ni kawaida kwa watu wengi kuvutiwa na nguo zinazowafanya waonekane wembamba zaidi ya maumbo yao.
3.Kuwa makini wakati wa kujiangalia kwenye kioo.
Mara nyingi vioo vya madukani huwa havina ukweli, ikiwa aina fulani ya nguo ilikuwa haikupendezi, haitakupendeza kamwe. Vinginevyo uwe umebadilika zaidi kimaumbile
Hizi ndizo hasa dondoo za jumla za mitindo ya kileo, lakini zaidi soma hapa;
Tumia rangi zinazokubali mapambo kwa urahisi, nazo ni; nyeusi, nyeupe pamoja na rangi nyinginezo. Mapambo hayo yanaweza kuwa ni pamoja na mikoba, viatu na hereni.
Hata hivyo, ikiwa una shingo fupi pendelea kuvaa mitindo ya kola ya wazi au shingo ya V, hii itasaidia kuifanya shingo yako ionekane ndefu ya kutosha. Pia unashauriwa kuvaa mkufu mrefu shingoni.

Wapendwa nawaombeni mnisaidie nielewe vizuri swala la mavazi maana siku hizi naona wachungaji hawazungumzii tena suala la mavazi kwa mkristo hasa huku mjini. 

Ninaona wakristo wakivaa nguo zisio na heshima wala maadili sio mitaani tu bali sasa wanaingia nazo kwenye ibada. 

Nijuavyo mimi wapendwa vazi kwa mwanamke ni muhimu sana. Maumbile ya mwanamke siku zote yanagusa hisia za mwanaume aliye kamili. 

Tukisema kwamba tumeendelea sana au tuko kiroho sa

na kiasi kwamba wadada hata wakivaa nguo zinazoonesha maungo yao haitusumbui sidhani kama ni kweli.Naamini kila mwanamme aliye kamili akiwa katika ibada akaona mazingira ya uvaaji nilioutaja hapo juu itamsumbua nafsini mwake. 

Nauliza wanawake kuvaa kwa kuzingatia viwango vya biblia ni ushamba au kuptwa na wakati?. Nawaombeni kama ni mimi nina shida mnielimishe wapendwa.

MAHUSIANO




Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!

Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..


Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida… Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.

2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao. 


3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……


4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.




5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi. 


6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..

7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..

SIYO KILA DALILI YA MWANAUME KUPENDA NI YA KWELI....!


Siyo kila dalili ya mwanaume kupenda ni ya kweli…!


Kuna wakati ambapo, wanawake wanajikuta wakikabiliwa na swali la, je, mwanaume huyu ananipenda kweli? Hii hutokea pale anapokutana na mwanaume ambaye, huenda amevutiwa naye. Pengine mwanaume naye anaweza kuonesha kuvutiwa na mwanamke huyo.

Kwa hiyo, mwanamke hujiuliza kama akubali ombi la mwanaume huyo na kukubali kuzungumza naye au kuanzisha naye uhusiano, kama mwanaume atakuwa amezungumza naye kuhusu jambo hilo. ni kweli kwamba, kuna ugumu kwa mwanamke kujua hasa ni kwa namna gani anaweza kujua kwamba, huyo mwanaume amempenda kweli au hapana.

Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa ni dalili ya kumpenda mwanamke, lakini wakati huo huo vinaweza visiwe.

1. Hebu tuchukulie kwamba, mwanaume ameonesha kuwa na tabia tunazoziita nzuri. Labda amekumbuka kirahisi jina la mwanamke, ameonesha kuwa msikilizaji mzuri, ameonesha kuwa anajali kuhusu kinachosemwa na mwanamke, na amekuwa anamuuliza maswali kwa dhati na utulivu. Hapa mwanamke anaweza kuamini kwamba, huyu mwanaume anampenda. Lakini ukweli huenda ukawa ni kinyume chake. Inawezekana huyo mwanaume ni muungwana tu, na anaonesha tabia hizo kutokana na uungwana wake na siyo kutokana na kumpenda kimapenzi mwanamke.

2. Kuna watu ambao wana upendo, wamekomaa kihisia na wanajua kuhusiana vizuri na watu. Hii haina maana kwamba, kumwonesha mtu tabia hizo, kuna maana ya kumpenda au kumpenda sana mwanamke. Dalili hizi ni nzuri na inawezekana zikawa zinaonesha mwanaume kumpenda mwanamke, lakini mwanamke asilichukulie jambo hilo kwa namna hiyo.

3. Mwanaume anaweza kuonesha kuwa na udadisi kuhusu mwanamke kwa maana kwamba, kutaka kujua mambo yake, kumfuatilia au kuulizauliza kuhusu habari za mwanamke. Hii haina maana kwamba mwanaume amempenda kimapenzi. Inawezekana mwanaume akawa amevutiwa kimapenzi na mwanamke ndiyo maana akaonesha tabia hizo, lakini siyo lazima iwe hivyo. Kumbuka kwamba, mwanaume anaweza kuvutiwa na mazungumzo ya mwanamke, akavutiwa hata na namna alivyo usoni, hivyo akapenda kuzungumza naye lakini siyo kwa sababu anampenda.

4. Kuna wanaume ambao wana wake au wapenzi, lakini wanajisikia vizuri kusikiliza wanawake wengine au kujua tu habari za wanawake wengine, bila kuwa na haja ya kuanzisha uhusiano nao. Mwanaume anapompa mwanamke ‘ofa’ hasa ya chakula cha mchana au usiku, ni dalili ya wazi ya kuvutiwa naye. Hapa kuna uhakika mkubwa zaidi, labda tu kama mazungumzo yanayotajwa kufanywa wakati huo wa chakula yanafahamika, na ni ya shughuli maalum. Kwa hiyo ‘ofa’ ya chakula ni dalili nzuri na yenye uhakika. Lakini kuna jambo ambalo ni muhimu kwa mwanamke kulifahamu katika hali kama hii. Kuna wakati mwanaume kumpa ‘ofa’ mwanamke kwa chakula cha mchana au jioni, kunaweza kusiwe na maana ya moja kwa moja kwamba, uhusiano utaundwa. Inawezekana katika kutoka outing huko, mwanaume akaghairi. Kwa wengine huchukua muda hadi kuamua kuhusu kuunda uhusiano au hapana.

5. Hata mwanaume kuamua kumpeleka mwanamke kwa familia yao na kumtambulisha kama rafiki yake, ni hatua yenye kuonesha kwamba, mwanaume ameamua kumpenda mwanamke huyo. Lakini wakati mwingine hii inaweza ikawa ni janja yake kutaka tu kumthibitishia mwanamke ili amhadae vizuri, na wala hakuna maana ya uhusiano wa kudumu.

6. Kuzungumza kwa pamoja kuhusu masuala ya baadaye ya kiuhusiano, kama vile, idadi ya watoto na mambo mengine ambayo mara nyingi huzungumzwa na watu ambao tayari wako kwenye uhusiano ni dalili ya mwanaume kuvutiwa mwanamke. Lakini tatizo la jambo hili ni kwamba, kuzungumza masuala ya baadaye inaweza kuwa ni njia ya mwanaume kutaka kujisikia au kujua jinsi inavyokuwa katika mambo hayo. Inaweza kuwa pia ni njia yake ya kutaka kupima wanawake wanavyosema kuhusu masuala hayo. Lakini inaweza ikawa mwanaume huyo anatafuta kujua misimamo ya mwanamke huyo ili hatimaye afanye uamuzi. Kwa hiyo, bado haioneshi kuwa amevutiwa na kuamua tayari.

Mara nyingi wanawake hudanganywa na dalili fulani zinazooneshwa na wanaume wakati wanapoanza kuzoeana nao. Dalili hizi huwafanya kuamini kwamba, wanaume hao wamewapenda tayari, wakati siyo kweli. Kwa kuangalia baadhi ya dalili hizo kama nilivyozitaja, mwanamke anaweza kuwa makini wakati anapoanzisha uhusiano, ili asikurupuke na kujikuta amedanganyika. Ni kweli, kuna wakati ni dalili zinasema kweli, lakini kuna wakai zinadanganya kuhusu kupenda au kupendwa.

JUL 26, 2013

WANAUME HAWAOI SURA TENA BALI UELEWA....!

Wanaume hawaoi sura tena bali uelewa…!

Siku za nyuma, wanaume walijali zaidi uzuri wa sura na mwili wakati walipokuwa wanatafuta mke. Lakini utafiti uliofanywa duniani kote unaonesha kwamba, wanaume hivi sasa wamebadili mitazamo na kuanza kuangalia vitu vilivyo zaidi ya uzuri wa sura na mwili.


Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Grand Valley kilichopo jimboni Michigan nchini Marekani walioendesha sehemu kubwa ya utafiti huo wamesema, wanaume hivi sasa wameanza kujali uwezo wa wanawake katika kufikiri na kujua namna ya kujenga maisha kuliko kujali sura zao na maumbile.



Tafiti nyingi, ukiwemo huo wa karibuni wa Chuo cha Grand Valley, zinaonesha kwamba, kwenye miaka hadi 1980, wanaume walikuwa wakioa wake ambao wanaume hao wanawazidi kielimu na hata kimapato. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi walikuwa wameoa wanawake ambao wanawazidi kielimu, kimapato au kukaribiana.



Lakini pia imebainika kwamba, hadi kufikia miaka hiyo, wanaume na jamii nyingi zilikuwa zikimtazama mwanamke anayefaa kuolewa kuwa ni yule mzuri sana kwa sura na umbo. Lakini kufikia mwaka 2002, wanaume wengi na jamii walikuwa wanaamini kwamba, mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa maisha ndiye anayefaa kuwa mke.
Kwa miaka ishirini hali imebadilika sana. Maisha yamezidi kuwa magumu na uhitaji wa watu kusaidiana katika kuyakabili umeongezeka. Kwa hiyo mtu anapofikiria kuoa huanza kujiuliza atakavyomudu maisha na mke. Kwa hofu za kushindwa, hujikuta akijiuliza namna atakavyoweza kusaidiana na huyo anayetaka kumwoa katika kufanya mambo yaende.


Siku za nyuma, mwanamke mwenye kipato kizuri alikuwa katika ugumu wa kupata mume, lakini siku hizi, bila kujali sura au sifa nyingine, uhakika wa mwanamke kuwa na njia za kipato unampa, nafasi kubwa zaidi ya kuolewa. Kilichokuwa kinaogopwa huko nyuma na wanaume kwa sasa ndicho kinachokimbiliwa.



Tafiti hizo zinasisitiza kwamba, thamani ya mwanamke kwenye jicho la mwanaume inaanza kuondoka kwenye uzuri wake wa sura na mwili na kuingia kwenye uwezo wake katika kuyakabili maisha. Hii ikiwa na maana kwamba, kwa kadiri siku zinavyoenda, wanawake ambao watakuwa na nafasi kubwa ya kuolewa watakuwa ni wale waliosoma au wale wenye shughuli za kuzalisha.

Wataalamu wengi wanasema, hivi sasa uzuri unaonekana kabisa kubadilishana nafasi na elimu na uwezo wa ‘kutafuta maisha’ wa mwanamke. Kwa hiyo, sasa siyo suala la uzuri tena, bali mwanamke anajua kitu gani na ana uwezo kiasi gani wa kufanya maisha yawe bora sana.


Hii pia ina maana kwamba, dhana ya zamani ya mwanamke mzuri kuolewa na mwanaume msomi au mwenye fedha imeanza kukosa mashiko. Siku za nyuma mwanamke mzuri sana, angeolewa na mwanaume mwenye fedha, kama zilivyo bidhaa nzuri kuangukia mikononi mwa wenye uwezo kifedha.



Lakini leo hii, wanaume wanachoweza kufanya ni kuwachezea kimapenzi wanawake wazuri na siyo kuwaoa. Linapokuja suala la kuoa, kisomo na uwezo wa kuyajua maisha huchukua nafasi. Uzuri wa sura hubaki nyuma kwanza.

WANAUME WENYE WAKE WAZURI, HUWA NA 'NYUMBA NDOGO' ZISIZOTAZAMIKA KWA SURA AU UMBO.....!

Wanaume wenye wake wazuri, huwa na ‘nyumba ndogo’ zisizotazamika kwa sura au umbo…..!

Kwa mujibu wa utafiti wangu nilioufanyia kwenye eneo langu la kazi na kwa majirani zangu nimebaini kwamba, kati ya wafanyakazi watano niliofuatilia nyendo zao, ni wawili ambao walikuwa na ‘nyumba ndogo’ nzuri na zenye mvuto kuliko wake zao. Watatu walikuwa na ‘nyumba ndogo’ ambazo zinaweza kumpelekea mtu kujiuliza inakuwaje mwanaume huyo kuwa na ‘nyumba ndogo’ hiyo ambayo hata kwa mbali sana haiwezi kulingana na mkewe. Kwa jirani zangu wanne hali haikuwa nzuri, kwani hapa watatu walikuwa na ‘nyumba ndogo’ zilizo kinyume na wake zao kwa sura na umbo.

Watu saba niliowahoji kuhusu jambo hili, watatu walisema kwamba, wana ushahidi kuhusu wanaume wanaowafahamu wenye ‘nyumba ndogo’ zisizotazamika ukilinganisha na wake zao. Wengine wanne walitoa ushahidi wa wanaume wanaowafahamu ambao wana ‘nyumba ndogo’ nzuri sana ukilinganisha na wake zao.


Ni kitu gani kinatokea?


Ni kwamba, kuna ukweli kuwa wanaume wanaweza kuacha wake zao wazuri sana nyumbani na kufuata wanawake wabaya wasiotazamika kwa sura na umbo huko nje. Lakini pia wanaweza kuacha wake zao wabaya kwa sura ndani na kwenda kufuata wanawake wazuri kwa sura na umbo huko nje.

Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba kuna mkanganyiko kwenye jambo hili. Lakini kwa bahati nzuri mkanganyiko huu kamwe siyo mkubwa na unaoweza kuumiza kichwa cha mtu. 


Binadamu ana kitu kiinachoitwa ukinaifu. Ukinaifu ni hali ya mtu kuchoka kukiona kitu kilekile mara zote. Kwa mfano, mtu anaponunua nguo mpya leo huipenda sana. Lakini baada ya muda fulani, ikiwa bado haijachakaa hujikuta kiwango cha kuipenda kikishuka.

Lakini ni vizuri nikarudi nyuma na kusema kwamba, kwenye suala la mapenzi. Ukinaifu huwapata wanaume kuliko wanawake. Inawezekana sababu ni za kimaumbile na hivyo ni vigumu kusema ni kwa nini inakuwa hivyo.


Kwa sababu ni suala la kimaumbile inakuwa kama lazima kwa mwanaume kupata ukinaifu. Anapopata ukinaifu siyo lazima atoke nje, yaani dawa yake au ufumbuzi siyo kutoka nje ya ndoa, ingawa wanaume wengi hufanya hivyo. Wanapofanya hivyo siyo kwamba, wanajua kwamba, wamepata ukinaifu, hapana. Wao hudhani tu kwamba, wamempenda mwanamke fulani kwa sababu hizi au zile.
Nadharia moja kuhusu ukinaifu ni kwamba, ili ukinaifu ushibishwe ni lazima mtu apate kitu kilicho kinyume na kile ambacho kimempa ukinaifu huo, au kuwa nacho mbali kwa muda fulani. Kwa mfano, kama mwanaume amepata ukinaifu wa umbile la mkewe ambaye ni kimbaumbau, ni lazima kama ataamua kwenda kutafuta mwanamke wa nje, atatafuta mwanamke tipwatipwa.

Kwa mkabala huo, ndiyo pale tunapokuta mwanaume akimfuata mwanamke wa nje mbaya ukilinganisha na mkewe. Labda anaamua kumfuata mwanamke huyo kwa msukumo wa ukinaifu – amekinaishwa na umbo au sura ya mkewe na hivyo angetaka kuona sura ya aina nyingine, ili afute ukinaifu wake. Kinyume cha sura nzuri ni sura mbaya, kwa hiyo atatafuta mwanamke mwenye sura kinyume na ile ya mkewe.
Kuna ukinaifu wa aina nyingi kwenye maisha ya ndoa. Mwanaume anaweza akakinaishwa na mtindo wa nywele wa aina moja wa mkewe. Kama mwanaume huyu hatakuwa mwangalifu, atajikuta akitafuta ‘nyumba ndogo’ yenye mtindo tofauti na mkewe. Inawezekana mkewe anatumia mtindo wa ‘twende kilioni’ kila akisuka nywele zake. Mwanamume anapokwenda kutafuta kilicho kinyume huko nje, anaweza akajikuta amevutiwa na mwanamke mwenye kunyoa na kuchana nywele zake fupi.

Kwa hiyo, inawezekana kabisa mwanaume akatoka nje ya ndoa yake kutafuta kinyume ambacho siyo sura wala umbile. Inawezekana akatoka kwa sababu amekinaishwa na ukimya wa mkewe, hivyo anatafuta kelele. Huyu anaweza kujikuta akiwa na mwanamke wa nje muongeaji na chakaramu sana, ambaye kisura na kiumbile anaweza kuwa sawa na mkewe.

WANAWAKE: WANAUME WANAPOWABISHIENI MSIWASHANGAE...!

Kwa nini wanaume ni wagumu sana kufanya mambo ambayo wake zao wanawaomba au kuwataka kufanya? Jibu, ni kwa sababu ni wanaume na wameona baba zao wakifanya hivyo na wakaiga. Lakini jibu linaweza kuwa lingine, kutegemea na ufahamu wa mtu na hata mazingira. Lakini ukweli unabaki kwamba wanaume sio wepesi wa kutenda yale ambayo wanatakiwa na wake zao kutenda. 

Taarifa za kiutafiti zinaonesha kwamba, mwanaume ni mgumu kufanya anayotakiwa au kuombwa na mkewe kufanya kwa sababu nyuma ya ubongo wake, kuna kizuizi. Inadaiwa kwamba ubongo wa kina wa mwanaume kuna kitu kinachopingana na chochote ambacho mwanamke anamtaka kufanya.



Siyo suala la kurithi, hapana. Ukweli ni kwamba, kutokana na mwanaume kutokuwa tayari kuongozwa au kumsikiliza mwanamke na kumkubalia, hatimaye imejijenga akilini na kuwa kama vile ni suala la maumbile. Ukweli ni kwamba, miaka mingi ya kutoamini kwamba, mwanamke anaweza, imefanya kuwe na kizuizi hicho kwenye akili ya mwanaume.

Utafiti wa hivi karibuni kwa mfano, ambao uliongozwa na Gavan Fitzsimons profesa wa masoko na saikolojia, kwenye chuo kikuu cha Duke, anasema, kinachotokea ni juhudi za mwanaume kutotaka kuingiliwa kwenye mambo yake, bila mwenyewe kujua kwamba, anafanya juhudi hiyo. Jambo hili kisaikolojia linafahamika kama reactance, ambapo mtu hufanya kinyume kabisa na anavyotakiwa kufanya. Ni juhudi za mtu kupinga kupewa amri au kuingiliwa katika uhuru wake. 

Wataalamu wanasema kwamba, wanaume hujikuta tu wamepinga jambo la mke bila kujua hata sababu. Ndio maana wanaume wengi huharibikiwa kwa kukataa kufanya yaliyopendekezwa na wake zao na baadae hujiuliza ni kwa nini walikataa. Kwa hiyo wanaume wanapaswa sasa kujua kwamba, wanapombwa jambo na wake zao au kutakiwa kulifanya, wako kwenye hatari ya kulikataa. Kwa hali hiyo, wanapaswa kuwa waangalifu.

JUL 10, 2013

MWANAMKE: JE UNATAFUTA MCHUMBA? FUATA KANUNI HII, HAKIKA UTAMPATA MCHUMBA MWENYE TABIA UZITAKAZO


Mwanamke: Je, unatafuta mchumba? Fuata kanuni hii hakika utapata mchumba mwenye tabia uzitakazo...

Kuna kitu kinaitwa nguvu ya mvuto, lakini pia huenda mmeshawahi kusikia au kusoma kitabu kinachoitwa “The Secret.” Ni kitabu kizuri sana kinachoeleza kwa kirefu na kwa lugha nyepesi inayoeleweka jinsi nguvu hii ya mvuto inavyofanya kazi. Katika kitabu cha The Secret mwandishi Rhonda Byrne anasema kwamba mawazo yetu ni kama sumaku. Kwa kawaida sisi wanadamu tumezungukwa na nguvu ambazo hatuzioni lakini zipo kwa hiyo Kwa jinsi tunavyofikiri hayo mawazo yanakuwa na nguvu ambazo zinavuta kila kitu tunachowaza, kiwe kizuri au kibaya, ni lazima kitarudi kilipotoka, ambapo sipengine bali kwako wewe mwenyewe.

Rhonda anazidi kubainisha utendaji wa mawazo yetu kwa kutoa mfano wa ufanyaji kazi wa Luninga (TV). Kama wote tunavyofahamu kuwa ili kituo cha kurusha matangazo ya Luninga kifanye kazi kunakuwa na minara inayosafirisha mawimbi na kuyageuza katika mfumo wa picha na hivyo kutuwezesha kuona matangazo ya luninga tukiwa majumbani kwetu. Wengi wetu hatufahamu mitambo hiyo inafanya kazi namna gani, lakini tunafahamu kwamba kila chaneli ina mawimbi yake ambapo kila tukichagua chaneli fulani tunapata picha katika luninga zetu. Tunachagua mawimbi kwa kubadilisha chaneli na ndipo tunapopata picha za matangazo kutoka katika chaneli hiyo. Kama tunataka kuona picha na matangazo tofauti katika luninga zetu tunabadilisha chaneli kwa kutafuta mawimbi ya chaneli nyingine.

Sisi kama wanaadamu tuko sawa na mnara wa kurusha matangazo ya luninga na tuna nguvu kuliko minara ya kurusha matangazo iliyowahi kuwepo hapa duniani. Mawimbi yetu ndiyo yanayoratibu maisha yetu na ndiyo yanayoifanya dunia iwe kama livyo leo, kwani tunatengeneza mawimbi kutokana na namna tunavyowaza. Ile picha tunayopata au tunayoiona kupitia mawazo yetu, sio sawa na ile tunayoiona katika luninga zetu sebuleni kwetu, bali ni picha ya maisha yetu! Mawazo yetu yanatengeneza mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza na kuwa ndio maisha yetu halisi.

Iwapo tunataka kubadili chochote katika maisha yetu, basi inatulazimu tubadili chaneli na mawimbi kwa kubadili namna yetu ya kufikiri. Mwandishi huyo anaendelea kusema, kinachosabisha watu wengi wasipate kile wanachokitaka maishani ni kwa sababu wanafikiria zaidi kuhusu kile wasichokitaka badala ya kile wanachokitaka. Hebu tujaribu kuchunguza mawazo yetu na kauli zetu, tutagundua siri kubwa. Kwani nguvu ya mawazo ipo na inafanya kazi. Ugonjwa mkubwa sana unaowakabili wanadamu hapa duniani karne kwa karne ni ugonjwa wa “sitaki” au “sipendi,” anabainisha mama huyo. “Watu wameendelea kuacha ugonjwa huu uendelee kutawala katika mawazo yao, vitendo vyao na kauli zao, wakiendelea kuzingatia yale wasiyoyataka au wasiyoyapenda.” Anamalizia kusema mwandishi huyo.

Ugonjwa huo ndio unaowatesa baadhi ya wanawake wanaotafuta wapenzi. Mfano halisi ni kauli kama, “mimi sipendi wanaume wafupi,” au “mimi sipendi kuolewa na mwanaume mnyanyasaji….” na kauli nyingine zinazofanana na hizo. Ukweli ni kwamba kitakacho watokea wanawake wenye kutoa kauli kama hizo ni kuishia kuolewa na wanaume wa aina hiyo….. kinachofanyiwa kazi na mawazo yetu ya kina (Unconscious Mind) ni kile tunachokitamka, iwe ndicho tunachokitaka au tusichokitaka, mawazo yetu ya kina hayajui neno sipendi au sitaki, hukuletea kile ulichokitamka na kukijaza katika akili yako. 


Kuna wanawake wengi ambao wameolewa au wamewahi kujenga mahusiano na wanaume ambao waliwahi kutamka hadharani kwamba kamwe hawatoweza kujenga mahusiano nao au kuolewa nao. Hayo ni matokeo ya kauli zao ambazo walizitamka bila kujua madhara yake. Kwa hiyo basi kwa kutumia kanuni hiyo ya mvuto kama alivyosema mwandishi Rhonda Byrne mnatakiwa kuanza kuratibu mawazo yenu na kauli zenu kwa kutamka aina ya wanaume ambao mngependa kujenga mahusiano nao au kuolewa nao na haiishii hapo ni vyema mkajiweka katika mazingira ambayo yatawavuta kuelekea mahali ambapo mtakutana na aina ya wapenzi muwatakao. Huwezi tu kukaa nyumbani kwako au kutembelea eneo moja hilo hilo kila siku halafu utarajie kukutana na aina ya mpenzi umtakaye itakuwa ngumu, labda uwe na bahati sana.

MWANAMKE: KABLA HAJATOA TAMKO LA KUFUNGA NDOA USIMWAMBIE HAYA...


Mwanamke: Kabla hajatoa tamko la kufunga ndoa usimwambie haya…!


Katika maisha wote tuna siri zilizotuzunguka na mambo mbalimbali ya kifamilia pengine yanayotia kinyaa ambayo huwa tunatamani yasijulikane kwa wengine au labda yafutike kabisa. Lakini inategemea unayachukuliaje mambo hayo au yanaathiri vipi mitazamo yako kuhusu wewe. Ukweli ni kwamba hatuwezi kuyabadili labda tunachoweza kufanya ni kubadili mitazamo ya wengine kuhusu yale yaliyotuzunguka…………

Familia yenu ni ya vurugu tupu:
Baba yako ni mlevi kupindukia au baba yako na mama yako wote ni walevi kupindukia. Kaka zako ni mateja au dada zako wote wamezalia nyumbani au waliwahi kuolewa na kuachika, na sasa wako nyumbani tu wakichapa umalaya na pengine wanaendelea kuzalia nyumbani. Haya ni mambo ambayo hupaswi kuyazungumzia kwa mpenzi ambaye hajatoa tamko la kutaka mfunge ndoa. Kwani itamfanya mpenzi mpya atengeneze tafsiri tofauti kuhusu wewe. 

Uhusiano wako wa mwisho na mwenzi wako ulivunjika kwa vurugu:
Inawezekana mpenzi wako wa kwanza mliachana kwa vurugu kubwa, kwa mfano ulifikia hatua ya kufanya jaribio la kunywa sumu kutokana na kugombana kwenu kabla ya kuachana kwenu. Haya ni mambo ambayo hupaswi kuyasema kwa mpenzi wako mpya, kwani utampa maswali mengi sana ya kujiuliza juu yako.

Idadi ya wapenzi uliowahi kuwa nao:
Kuwa na idadi ndogo au kubwa ya wanaume uliowahi kuwa na uhusiano nao haimaanishi kwamba wewe ni mzuri katika mapenzi, sana sana unajidhalilisha tu. 


Maisha yako ya ujanani ya kujirusha:
Maisha yako ya ujanani au ulipokuwa shule ukijirusha kwenye kumbi za starehe ni ya kwako na si vyema uyapigie upatu kwa mpenzi mpya ili akujue kwamba na wewe hauko nyuma katika mambo ya starehe.


Ushawahi kuishi maisha ya kutangatanga:
Ni kumbukumbu yenye kuumiza hisia pale ukumbukapo maisha yako ya utotoni kama yalikuwa magumu na machungu. Kulelewa na wazazi wasiojali na watesaji, kuishi kwa kutangatanga kutoka nyumba moja hadi nyingine kutafuta hifadhi kutokana na kunyanyaswa. Kubakwa au kuishi maisha ya vurugu katika familia. Haya ni matukio ambayo yameshapita na hayatakiwi yatawale fikra zako tena. Umeshakua mtu mzima na maisha yanasonga mbele. Kuanza kumsimulia mpenzi mpya kuhusu aina ya maisha uliyokulia kama yalikuwa ni ya taabu kama nilivyoeleza hapo juu kutamfanya akuone kama wewe utakuwa unatonesheka kihisia haraka kutokana na kujeruhiwa kihisia utotoni. Mpenzi anaweza kukukwepa na hatimaye kukukimbia.

JUL 8, 2013

HII NDIYO SABABU YA WANAWAKE WENGI KUIBUA MABOMU...!

Hii ndiyo sababu ya wanawake wengi kuibua mabomu…!

Mnamo mwaka 1973 Dk. Paul MacLean, mtafiti toka taasisi ijulikanayo kama National Instute of Mental Health, alibaini kwamba, ubongo una sehemu tatu zinazoendana na nyakati tatu za mabadiliko ya kimaumbile.

Sehemu ya kwanza inaitwa reptilian. Hii inahusiana na kukutana kimwili kati mwanamke na mwanaume na tabia ya ukatili, hisia za hasira na hofu. Sehemu ya pili ni limbic brain. Hii inahusika na mapenzi, huzuni na wivu. 

Hata matumaini asili yake ni katika sehemu hii. Sehemu hii ndiyo inayodhibiti mapigo ya moyo na joto. Yote haya huathiriwa na kuwepo mahali hapo na mtu tunayempenda. Hamu ya mapenzi huenda moja kwa moja katika sehemu hii. Ni sehemu ambayo ina pupa na inaenda kasi kama umeme.

Ni enao ambalo halitaki kabisa kujishughulisha na mambo ya kutumia akili au tathmini. Sehemu ya tatu ya ubongo inaitwa neo-cortex, ambayo huruhusu matumizi ya mantiki, kutafakari kwa kina, lugha, kufanya mipango, kufikiri na maamuzi ya kina baada ya kufikiri kwa kina.

Katika kitabu chake cha The Emotional Brain, Joseph LeDoux anasema kwamba, sehemu zile mbili za kwanza za ubongo zinathibiti sana ile sehemu ya tatu. Na wala hii sehemu ya tatu haina udhibiti kwa zile sehemu mbili. Na ndiyo maana katika maisha ya kawaida, ‘hisia hudhibiti fikra.’ 

Ingawa fikra zinaweza kuamsha hisia kirahisi, lakini fikra zinapata tabu sana kuziondoa hisia zikishaingia. Hii ina maana sehemu ya pili ambayo ndiyo inayoziamrisha hisia, inaweza kuiburuza sehemu ya tatu kila inapotaka. Limbic ya mwanamke itamwambia, “umempata mwanaume barabara.” Sawa, lakini mwanaume mwenyewe ni mlevi..! 
Limbic itasema, “Nitaishi naye hivyohivyo. Ana sura nzuri mno, ninajisikia vizuri sana ninapokuwa naye….”


Sasa nafikiri unaweza kuona kwamba, hata kama mwanamke anaweza kusema kwamba anamtaka mwanaume mwenye haiba nzuri na mtu mwema si lazima kwamba, ndiye atakayevutiwa naye. Mfano mzuri wa jambo hili ni chakula.

Je huwa tunakula chakula kufuatana na ubora wake kiafya? Hapana…! Wengi wetu tunakula kutokana na utamu na ladha ya chakula! Dona ni bora kuliko ugali wa mahindi yaliyokobolewa kiafya. Lakini asilimia 90 ya Watanzania wanapenda ugali wa mahindi yaliyokobolewa maarufu kama Sembe. 

Hali hii ndiyo inayompata mwanamke anapofanya uchaguzi na kujikuta akimchagua mwanaume anayemfanya kujisikia raha, lakini ambaye si mtu mzuri kwake.

Suluhisho la jambo hili ni nini….?

Wanawake wanaweza kufanya urafiki na wanaume hao wazuri wa sura na wenye sifa ya uburuzaji na valuvalu kwa idadi wanayotaka kama kwa kufanya hivyo watajisikia raha maishani mwao; ili mradi tu urafiki huo usilete maumivu na huzuni ambayo yako juu kuliko furaha yenyewe. 

Kama huzuni ni kubwa kuliko furaha katika mapenzi na mwanaume aliye naye, basi mwanamke hana budi kuachana na limbic brain na kuchagua mwanaume anayemfaa kwa kutumia mantiki.

KWA NINI WANAUME WENGI SIKU HIZI HAWAPENDI KUOA...?

Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano: Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

Mgogoro wa kiuchumi: Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.



Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu: Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego 
tu. 

Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha: Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.


Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto: Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa: Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.

UHUSIANO UNAPOVUNJIKA, WANAWAKE NDIYO HUUMIA ZAIDI....!


Kwa kuangalia idadi ya watu wanaoathirika kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume mtu atagundua kwamba wanawake ndiyo ambao hupatwa na athari kubwa zaidi. Kwa mfano ukichukua watu ishirini, wanawake kumi ambao wameachwa na wapenzi wao na wanaume kumi ambao nao wameachwa pia na wapenzi wao, utagundua kwamba, wakati ni wanaume watatu tu kati ya hao kumi ndio watakaosumbuliwa sana na na hali hiyo, kwa wanawake idadi itakuwa ni saba kati ya hao kumi. 


Watu wengi wanaweza kukimbilia kwenye kusema hali hiyo inatokana na utegemezi wa wanawake kwa wanaume. Hii ikiwa na maana kwamba, wanaathirika zaidi kwa sababu, kwa kuachwa ina maana pia kwamba hawataweza tena kupata mahitaji ambayo walikuwa wanapewa na wanaume hao. Dhana kama hii inaweza kuwa na ukweli fulani, lakini hali halisi inakataa. Kuna wanawake ambao wana uwezo mkubwa nap pengine ndiyo wanaowalisha na kuwavisha wanaume, lakini wanapoachwa na wanaume hao huathirika sana. 

Wanawake wa aina hii inadaiwa kwamba huathirika zaidi kuliko wale walio tegemezi. Kuathirika huku kwa ziada huhusishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba wanaume ni watu wa kutoa ili kupalilia penzi, lakini hapa badala ya kutoa wanapewa na bado wanaondoka. Hili huwatanza wanawake wa aina hii. Lakini sababu ambayo huenda wengi wetu tulikuwa hatuijui kuhusiana na suala hili la wanawake kuathirika zaidi baada ya kuvunjika kwa penzi au kuachwa ni ‘ndoto.’ Kimaumbile wanawake huota zaidi ndoto za mchana au hufikiria zaidi kuhusu maisha yao ya kimapenzi yatakavyokuwa ukilinganisha na wanaume. Siyo kufikiria tu, bali hufikiria kwa njia inayoonyesha kuwa maisha hayo yatakuwa kama peponi.



Wanawake, wakiwa bado wasichana (baada ya kuvunja ungo) huanza kufikiria na kupiga picha jinsi busu lao la kwanza litakavyokuwa, mtu ambaye watabusiana awali. Hufikiria pia kuhusu wapenzi wao wa awali watakavyokuwana jinsi itakavyokuwa watakaposhiriki nao tendo kwa mara ya kwanza na huwa wanapiga picha ya jinsi siku yao ya harusi itakavyokuwa na watu watakaowaona. Katika kupiga picha huko huwa wanafikiria namna ambavyo mambo hayo yote yatakavyoenda vizuri bila doa, huwa wanajiona wakiwa wamefanikiwa katika hatua zote na hatimaye kuishi kwa raha mustarehe milele na watakaokuwa wapenzi wao. Kwa upande wa wanaume hakuna ndoto za aina hii na hata kama zipo ni kwa wachache sana, wakati kwa wanawake ni kama sehemu ya makuzi kwao. 


Kwa hali hiyo, ukiacha mazingira wanamokulia wanawake, kwa sehemu kubwa hukua wakiwa na hizo ndoto zao, ambazo kwao siyo ndoto bali ukweli. Wanapokuja kwenye ukweli wa uhusiano hugundua kwamba busu la awali siyo kama walivyotegemea liwe, mpenzi wa awali siyo kama walivyomtegemea awe na wala maisha ya ndoa siyo matamu kama walivyokuwa wameota. Kwa kuwa hawakujiandaa wala kutegemea mazingira magumu ya uhusiano, hawakuwa wakiota kuhusu ugumu wa uhusiano bali wororo, wanapokutana na masuala ya kuvunja moyo kama kuachwa hubabaika sana. Kwa kuwa akilini mwao walikuwa na picha ya mafanikio katka uhusiano, kushindwa kwa uhusiano, huwafanya wajione kwamba, wao ndiyo wakosaji, wameshindwa kulinda uhusiano ambao katika ndoto zao waliamini kwamba ni mzuri na usio na doa 


Ukiangalia kwa makini katika uhusiano, wanawake ndio wanaojitahidi sana kulinda uhusiano usivunjike, wao ndiyo wavumilivu zaidi, ndiyo ambao hujitahidi kuyarudisha mambo yaende sawa pale yanapokwenda kombo hata kama kufanya hivyo kunawagharimu. Yote hii ni juhudi yao ya kutaka kuishi kwa kadiri ndoto zao za kabla zilivyowaonyesha, kwamba uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume ni mtamu, mororo na usio na chembe ya doa……