Mavazi kwa mwanadamu ni suala lenye umuhimu mkubwa lakini kwa mwanamke lina umuhimu wa kipekee siyo tu ili kuboresha mwonekano wa mhusika, bali pia kueleza haiba yake.
Ni wazi kuwa itakuwa kazi rahisi kumwelezea mwanamke husika alivyo kwa kumtazama namna anavyovaa, hivyo unaopaswa kuelewa ni kwamba mitindo ina nafasi kubwa katika kueleza tabia na mwenendo wa kila siku wa mtu .
Katika hilo wanawake wanatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kujipamba na wakati mwingine husifiwa kwa kuwavutia wengine kuwa watanashati.
Pamoja na sifa hiyo wanawake hufanya makosa mbalimbali katika uvaaji. Hii mara nyingi hutokana na uelewa mdogo katika suala zima la uvaaji.
Je, unapenda kufahamu dondoo mbalimbali za uvaaji? Soma hapa:
1. Unapojaribisha nguo, hakikisha umesimama wima pia jiweke katika pozi tofauti. Kwa kufanya hivyo utaweza kugundua urefu wako, pia utajionea unavyovutia katika vazi husika.
2.Elewa umbo lako linavyovutia. Ni kawaida kwa watu wengi kuvutiwa na nguo zinazowafanya waonekane wembamba zaidi ya maumbo yao.
3.Kuwa makini wakati wa kujiangalia kwenye kioo.
Mara nyingi vioo vya madukani huwa havina ukweli, ikiwa aina fulani ya nguo ilikuwa haikupendezi, haitakupendeza kamwe. Vinginevyo uwe umebadilika zaidi kimaumbile
Hizi ndizo hasa dondoo za jumla za mitindo ya kileo, lakini zaidi soma hapa;
Tumia rangi zinazokubali mapambo kwa urahisi, nazo ni; nyeusi, nyeupe pamoja na rangi nyinginezo. Mapambo hayo yanaweza kuwa ni pamoja na mikoba, viatu na hereni.
Hata hivyo, ikiwa una shingo fupi pendelea kuvaa mitindo ya kola ya wazi au shingo ya V, hii itasaidia kuifanya shingo yako ionekane ndefu ya kutosha. Pia unashauriwa kuvaa mkufu mrefu shingoni.
No comments:
Post a Comment