Tuesday, October 21, 2014
Toto yaendeleza wimbi la ushindi
Kikosi cha maafande wa Green Warriors toka Dar es Salaam wakati wa mapumziko wakipata nasaha ili kurudisha bao 2-0 walizofungwa na Toto Afrikan katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mchezaji Ladislaus Mbogo akihakikisha apiti mtu
Mwamuzi wa mchezo huo Ezekiel Mboi toka Shinyanga akifuatilia kwa kina mchezo
Beki Wazir Ally akimdhibiti nahodha wa Green Warrior Edward Heri
Kocha msaidizi wa Toto Afrikan Nicholaus Mkumbaili akimwelekeza Mwita Kimaronge baada ya kushindwa kuipatia goli licha ya kupoteza nafasi tano za wazi
Mchezaji Keneth Heri ambaye alizua tafrani mnamo dakika ya 62 baada ya kumvaa mwamuzi wa pembeni Justina Charles toka Tabora na baade kuamua kujitoa mwenyewe uwanjani bila kuzawadiwa kadi nyekundu
Mfungaji wa mabao mawili ya Toto Afrika Jaffari Mohammed aaliyesajiliwa toka Polisi Tabora, akishangilia baada ya kuipatia bao la pili mnamo dakika ya 42
Toto imefanikiwa kushinda mechi zote tatu za nyumbani baada ya kuichapa Mwadui ya Shinyanga 1-0, Burkina Fasso ya Morogoro 2-1 na Green Warriors 3-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment