Tuesday, October 21, 2014

Bodi ya ligi yakanusha kumzawadia Mwambusi




Bodi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara TPL Board imekanusha taarifa za kumzawadia tuzo ya kocha bora wa mwezi, kocha mkuu wa klabu ya Mbeya City Juma Mwambusi kabla ya mchezo wa ligi uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa juma lililopita.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi TPL Board Sailas Mwakibinga amesema taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ambazo  zinadai bodi hiyo ilimzawadia mwmabusi tuzo ya kocha bora wa mwezi hazina ukweli wowote zaidi ya upotoshaji ambao wanaamini umetokana na mkanganyiko uliojitokeza uwanjani hapo kabla ya mchezo dhidi ya Azam FC ambao walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
                                                 Juma Mwambusi

Mwakibinga amesema kilichofanyika mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa Sokoine ni utoaji wa zawadi ya tuzo ya mchezaji bora wa mwezi na tuzo ya kocha bora wa mwezi kama ilivyofahamishwa kwa wadau wa soka nchini kote kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii.

Hata hivyo mwakibinga amezungumzia kizungumkuto kingine ambacho kimejitokeza kwa wadau wa soka kuhoji kwa nini walimtunuku tuzo ya mchezaji bora Anton Matogolo na si Didier Kavumbavua mbae kwa mwezi Seoptemba alioenkana kuwa na uwezo mkubwa kutokana na kasi ya upachikaji mabao aliyoanza nayo tangu msimu huu.

Mwakibinga hakuishia habo bali ameendelea kutoa ufafanuzi wa kina ambao unaiwezesha ligi hiyo kupata tathmini ya uhakaka kutoka katika viwanja vinavyotumika kwa ajili ya michezo ya ligi kuu ya soka tanzani abara msimu huu, na kufikia hatua ya kumpata mchezaji bora wa mwezi.

No comments:

Post a Comment