Mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISETA) ngazi ya mkoa yameanza kushika kasi kwa kuzikutanisha timu zote za wilaya saba za mkoa wa Mwanza katika viwanja vya shule za Sekondari za Nsumba na Ngaza.
Mashindano hayo, ambayo yanatazamiwa kutoa ushindani
mkali kwa washiriki kutoka wilaya ya Nyamagana ambao walikuwa mabingwa msimu
uliopita na mahasimu wao wilaya ya Ilemela waliomaliza nafasi ya pili.
Akizungumza na mwandishi wetu, Afisa habari wa Ilemela
Bahati Kizito alisema kuwa, kwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanatwaa
ubingwa wa mkoa ili kuonyesha kuwa wanaweza michezo licha ya uchanga wa wilaya
yao kwani mashindano
ya mwaka huu ni ya tatu toka kuanzishwa kwa halmashauri hiyo
.
“Msimu uliopita tulimaliza nafasi ya tatu ila msimu
huu tumejipanga kumaliza nafasi ya kwanza, pia kutoa wachezaji wengi
watakaowakilisha mkoa katika mashindano ya kanda”alisema Kizito.
Na kuongeza kuwa, tayari wameahidiwa na Raisi wa
zamani wa chama cha mpira wa wavu Musa Mzia, kupatiwa jezi kwa wachezaji wa
mpira wa kikapu kila watakapo kuwa wakifanya vizuri katika mashindano kwa
mchezo huo.
Pia alizitaja changamoto kubwa zinazowakabili kuwa ni baadhi
ya shule hasa za Serikali kutoshiriki katika mashindano haya, hivyo kuwanyima
fursa wanafunzi wao kuonesha vipaji pamoja na ukosefu wa vifaa vya michezo.
Mashindano
hayo yanashirikisha michezo ya mpira wa
miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono, riadha, meza yote kwa
wasichana na wavulana huku bao ni wavulana na mpira wa pete ni kwa wasichana
pekee.
Kwa upande wa wilaya ya ilemela jumla ya wanamichezo 125 na viongozi na
walimu 12 wanashiriki michuano hiyo,
iliyoanza kutimua vumbi siku ya leo (Alhamisi).
Wilaya ya Ilemela mwaka 2013 ilishika nafasi ya pili kati ya
mikoa saba iliyoshiriki, huku mwaka 2012 ilishika nafasi ya mwisho.
Huku mabingwa watetezi jiji wakiahidi kuendeleza
ubabe kwa msimu huu, kwa kushinda zaidi ya msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment