Waandishi watatu wa Mwananchi wahitimu mafunzo ya Mazingira
ya kibiashara
Mwanza:
Waandishi watatu kati ya kumi waliohudhuria
mafunzo hayo yaliyodumu kwa mwaka mmoja,
kutoka kampuni ya Mwananchi wamehitimu mafunzo hayo jana yaliyokuwa yakiendeshwa Chuo kikuu cha
Mtakatifu Augustine(SAUT) kwa kushirikiana na Best AC na Ansaf.
Waaandishi hao ni Stella Ibengwe kutoka Shinyanga, Mariam
Juma kutoka Mwanza na Felix Lazaro kutoka The Citizen Dar es Salaam huku
wengine wakiwa ni Nancymona Ijumba kutoka Redio SAUT, Moses Mathew kutoka Daily
News, Suleiman Shagata kutoka Baruti, Mobin Sarya kutoka Zenji Media, Johnson
Matinde kutoka Clouds Fm, Fadhili Abdallah kutoka Habari Leo na Anna Ruhasha
kutoka Sauti ya Afrika.
Akizungumza katika hafla hafla hiyo fupi, naibu meneja mradi
wa Best AC, Ali Mjella alisema kuwa, kundi hili ni la pili toka kuanza kwa mafunzo
hayo ambayo yamekuwa na changamoto nyingi ila bado wataendelea kuyatoa kwa
miaka mitano ijayo ili kuboresha sekta ya uchumi na biashara.
“Mafunzo yataendelea na uboreshwaji zaidi utafanyika kuanzia
July mwaka huu na itaitwa Best Dialogue, licha ya changamoto tuliyoipata katika
kundi lililopita ambao wengi walipandishwa vyeo katika kitengo tofauti kwa wao
ni furaha lakini kwetu ni changamoto kwani lengo ni kuzalisha waandishi wa
habari za uchunguzi vijijini katika
mazingira ya biashara na kilimo”anasema Mjella.
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo, mkuu wa chuo cha SAUT,
Thadeus Mkamwa aliwaasa waandishi hao kutokuwa kama kengele ambayo bila
kugongwa haina maana yoyote.
“Kengele aisifiwi mpaka igongwe, vivyo hivyo kwa mwandishi
au mtangazajia hawezi kusufiwa mpaka alete mabadiliko katika jamii, tumeanza
mafunzo July 2013 na leo Mei 23, 2014 tumehitimu lakini lengo letu kubwa ni
kuona mazingira ya kibiashara yanaboreka zaidi kupitia nyie kwa kuandika habari
zenye weledi na zenye lengo la kuelezea ukweli kwa takwimu”anasema Mkamwa.
Goodluck Urassa mhadhili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam
akizungumza kwa niaba ya wahadhili waliotoa mafunzo hayo, aliwataka wahitimu
hao kuanza kutekeleza majukumu yao mara moja na kuacha ile tabia ya kila siku
najipanga kwani lengo la mafunzo hayo ni
kuwekwa katika vitendo ili kuleta mabadiliko ni si kubaki katika nadharia.
Huku mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge akiwataka waandishi
hao kuwakomboa wakulima ambao wanaishi katika mazingira magumu licha ya
kuwalisha watu wa rika zote nchini.
“Mwandishi ni sehemu muhimu ya uchechemuzi, hivyo ANSAF wapo
tayari kuwasaidia wale ambao wanahitaji msaada wa kitaalamu katika masula ya
kilimo na bajeti ili kuona ni kwa kiwango gani wanaweza kumkomboa mkulima wa
kijijini”anasema Audax.
Aidha katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa na Stella Ibengwe,
ilitaja changamoto zilizowakabili hivyo kuomba kutatuliwa kwa lengo la
kuboresha mafunzo hayo awamu ijayo.
“Tunaomba mafunzo yajayo muongeze vipindi vya nadharia
darasani hasa katika utafiti, habari za uchunguzi, uchambuzi na uandishi wa
habari kuhusiana na ripoti zilizochzpishwa, uchambuzi kuhusiana na masuala ya
kibiashara na mwenendo wa kiuchumi lakini pia kuweza kuwapatia vitendea
kazi washiriki kama vile vinasa sauti,
tarakishi mpakato na kamera”ilisema riasala hiyo ambayo iliahidiwa kufanyiwa
kazi katika mafunzo yajayo.
No comments:
Post a Comment