Wednesday, May 21, 2014

SHINDANO LA MAMISS SHINYANGA




WASHIRIKI WA MISS SHINYANGA KATIKA PICHA YA PAMOJA WAKATI WA MAZOEZI
 MASHINDANO  ya kumsaka miss Shinyanga Centre yanatarajiwa kufanyika mei 23 mwaka huu, huku warembo 10 watapanda jukwaani kugombea taji hilo kwa mwaka 2014.
Licha ya mashindano hayo maandalizi yake kukamilika lakini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo idadi ya washiriki kuwa ndogo,kutokana na baadhi ya wazazi kuwazuia watoto wao kushiriki kwa madai kuwa ni uhuni hivyo kupelekea idadi ya washiriki kuishia 10 na kushindwa kuleta changamoto kubwa.
Muuandaaji wa mashindano hayo Elizabeth Stephen,anawaomba wazazi pindi mashindano kama hayo yakitokea wawaruhusu  mabinti zao   kushiriki zoezi la kumsaka miss shinyanga centre, kwani umiss ni fani na ni kipaji kama ilivyo kwa vipaji vingine vya wachezaji wa mpira wa miguu na pete.
“ mpaka sasa kuna warembo kumi tu ambao wanashiriki kinyanyanyiro hicho, hivyo ni vema wazazi wakawaruhusu mabinti zao ili kuleta changamoto kwa washiriki, badala ya ilivyo sasa idadi ni ndogo haina changamoto kubwa”alisema muandaaji huyo Elizabeth.
Baadhi ya washiriki wa miss shinyanga centre Grace Kimaro Yunice Kidaha walisema   hakuna uhuni ndani ya zoezi la umiss bali uhuuni ni tabia ya mtu, hivyo wazazi wawaruhusu watoto wao ili waweze kusrikiki mashindano.
 Hata hivyo washiriki wote kwa nyakati tofauti kila mmoja alijigamba kutwaa taji hilo kwa kuwamwaga wengine,ambapo walibainisha kuwa mshindi atakaye ibuka kutwaa taji hilo atatoa kipaumbele kwa jamii kuielimisha kuachana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBONO ) na vikongwe.

No comments:

Post a Comment