Friday, November 21, 2014

MAKOCHA WANOLEWA


Makocha wa soka nchini wametakiwa kuzingatia taaluma zao kwenye mchezo huo na kuachana na masuala ya unazi na siasa michezoni kwani kufanya hivyo kunadumaza mchezo wa soka nchini.
Ushauri huo kwa makocha wa soka nchini umetolewa na makamu wa raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Walace Karia wakati akifunga  kozi ya makocha leseni C ya siku 14 iliyofanyika mkoani Morogoro kwa kuwashirikisha makocha kutoka ya mashariki.

Kwa upande wake katibu wa chama cha makocha mkoa wa Morogoro (TAFCA) Ahamed Mumba amewasisiti wahitimu wa kozi hiyo kutumia uweledi na mbinu za kitaalum pale inapojitokeza mambo kuwaendea tofauti, na si kuingizwa katika ushawishi wa kufanya mamboa mbayo hayaendani na soka.

Nae kocha mkongwe Mohamed Msomari amelitaka shirikisho la soka nchini pamoja na viongozi wa baadhi ya klabu, kuacha mpango wa kuwafikiria makocha wageni kwenye timu za taifa na badala yake wahakikishe wanatoa kipaumbele kwa makocha wazawa.

Pia ammesisitiza suala la kuheshimiwa kwa taalum ya ukocha nchini, na kuitaka itazamwe kama nafasi nyingine za kazi, kwa kuhakikisha makocha wanapata heshima na kulipwa stahiki zao kwa wakati.

Wakati huo huo mmoja wa  mshauri wa kocha wa Standa Utd inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara Muhibu Kanu amewataka makocha wenzake kuhakikisha wanazingatia maadili ya taaluma wanayoendelea kuipata kupitia kozi mbali mbali zinazoendeshwa nchini kote.

Kozi hiyo ya makocha Leseni C, ilianza Novemba tano na kuendeshwa na mkufunzi Sunday Kanyuni ikiwa ni mpango wa TFF kwa kushirikiana na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambayo yataendeshwa kwa kila kanda.

No comments:

Post a Comment