Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa
ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa kushuhudia michezo kumi katika
viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.
Mkurugenzi wa mashindano wa TFF amesema michezo ya ligi hiyo imesogezwa
mbele ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha
timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe,
Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.
No comments:
Post a Comment