Mabingwa wa soka barani Afrika timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles wameshindwa kufuzu kucheza fainali za mwaka 2015 ambazo zimepangwa kufanyika Equatorial Guinea badala ya Morocco walioamua kuipiga teke nafasi ya kuwa mwenyeji.
Nigeria wameshindwa kufuzu kufuatia matokeo ya sare ya mabao
mawili kwa mawili waliyoyapata usiku wa kuamkia hii leo, walipocheza nyumbani katika
uwanja wa Akwa Ibom, huko mjini Uyo dhidi ya kikosi cha Afrika kusini Bafana
Bafana.
Katika mchezo huo kikosi cha Nigeria kilitakiwa kusaka
ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutetea ubingwa wake kwa mwaka ujao
kutokana na uwiyano wa point saba uliokuwepo kati yao na timu ya taifa ya Congo
Brazzaville.
Endapo Nigeria wangeshinda wangefikisha point kumi na
wangebebwa na uwiyano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, lakini imekua
tofauti na badala yake Congo Brazzaville walifanikiwa kuwabanjua Sudan bao moja
kwa sifuri na kufikisha point 10 huku wakiwaancha Super Eagles wakiwa na point
nane.
Michezo mingine ya mwisho ya hatua ya makundi ya kusaka
tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika iliyochezwa usiku wa kuamkia hii
leo kwa upande wa kundi la pili:
Ethiopia 0-0 Malawi
Mali 2-0 Algeria
Kundi la
Tatu.
Burkina Faso 1-1
Angola
Gabon 4-2 Lesotho
Kundi la
Nne
Ivory Coast 0-0
Cameroon
DR Congo 3-1 Sierra
Leone
Kundi la Tano
Ghana 3-1 Togo
Guinea 2-0 Uganda
Kundi la Sita
Niger 1-1
Mozambique
Zambia 1-0 Cape
Verde
Kundi la Saba
Senegal 3-0
Botswana
Tunisia 2-1 Egypt
Kwa mantiki hiyo sasa timu zilizofuzu kucheza fainali za
mataifa ya Afrika za mwaka 2015 kuanzia Januari 17 hadi February 8 huko
Equatorial Guinea ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Congo Brazzaville, Congo DRC, Zambia, Gabon, Ghana, Guinea, Ivory Coast, Mali, Senegal, Afrika Kusini, Tunisia pamoja na Equatorial
Guinea (wenyeji).
No comments:
Post a Comment