Askari waliokua wanatekeleza jukumu la kuangalia usalama
katika uwanja wa Félix Houphouėt-Boigny,
huko mjini Abidjan ambao ulitumika kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kundi la
nne kati ya timu ya taifa ya Ivory Coast dhidi ya Cameroon walilazimika kutumia
nguvu baada ya mashabiki kuingia katika sehemu ya kucheza mara baada ya filimbi
ya mwisho kupulizwa na muamuzi Bouchaļb
El Ahrach kutoka nchini Morocco.
Hali ilionkena kuwa ya mtafaruku kutokana na furaha iliyokua
imepitiliza kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Ivory Coast, baada ya kuona timu
yao ikikata tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2015.
Mashabiki walifanikiwa kuvunja uzio unaotenganisha sehemu za
majukwaa na sehemu ya kuchezea na kwenda kushangilia sanjari na wachezaji wa
tembo wa pwani ya Afrika ya magharibi, lakini walionyesha kuvuka mipaka na
kufikia hatua ya kuwabugudhi wachezaji.
Mshambuliaji wa klabu ya AS Roma ya nchini Italia Gervais Yao Kouassi Gervinho ndie
alipata wakati mgumu zaidi kutokana na shabiki mmoja kumvagaa na kumkumbatia
lakini furaha ilipitiliza na kujikuta akitaka kumvua nguo mchezaji huyo.
Katika hali hiyo askari walilazimika kumuondoa lakini
alionekana kukaidi na ndipo alipoangushiwa kichapo kwa kupigwa na virungu.
Katika kundi la nne Ivory Coast wamepita baada ya kushika
nafasi ya pili sanjari na Cameroon wanaoongoza kundi hilo, lakini Congo DRC
walioshika nafasi ya tatu walifuatia kwa kupata nafasi ya upendeleo ya kuwa na
uwiyano mzuri wa point pamoja na magoli ya kufunga na kufungwa kuliko timu
nyingine yoyote iliyoshiriki kwenye hatua ya michezo ya kufuzu.
No comments:
Post a Comment