Michuano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 inayoshirikisha
kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30
mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.
Kila timu ya mkoa inatakiwa kuwa na ujumbe wa watu 16,
wakiwemo wachezaji 14 na makocha wawili katika michuano hiyo ya timu yenye
wachezaji saba (7 aside).
Timu zitatakiwa kuwasili jijini Mwanza kuanzia Desemba 28
mwaka huu tayari kwa ajili ya uhakiki wa umri na taratibu nyingine za michuano
na timu zote zitafikia katika shule ya Alliance (Alliance Schools).
Wachezaji wanaotakiwa kushiriki michuano hiyo ni wenye umri
chini ya miaka 12, hivyo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 2003 na kuendelea.
No comments:
Post a Comment