Tuesday, February 3, 2015




Bondia wa kulipwa nchini Tanzania, Francis Cheka, ambaye ni maarufu kwa jina la SMG, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumpiga meneja waje wa baa yake , Bahati Kibanda.
Cheka alitiwa hatiani Julai 2 mwaka jana kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali Kibanda ambaye alikwenda hapo kudai fedha zake katika baa aliyokuwa anaifanyia kazi ijulikanayo kwa jina la Vijana Social Hall.
Cheka anayeshikilia mkanda wa WBF alipandishwa Kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro, kwa shitaka hilo lililosomeka kuwa ni la shambulio la kudhuru mwili na kujeruhi.
Hakimu Mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya alikubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kuthibitisha shitaka hilo.
Cheka anadaiwa kutenda kosa hilo kwa Kabanda ambaye alikuwa ni Meneja wa baa yake ya Vijana Social iliyopo maeneo ya Sabasaba katika Manispaa ya Morogoro baada ya kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo.
Hakimu Msuya alisema kuwa adhabu hiyo ni fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao kwa watu wengine na anatakiwa kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh milioni moja.
Pamoja na Cheka kupewa nafasi ya kujitetea, bondia huyo hakutoa maelezo yoyote na kuiachia mahakama hiyo kutoa adhabu inayostahili kwa bondia huyo aliyejizolea sifa kemkem katika ngumi za kulipwa nchini.
Hata hivyo, familia ya Cheka inampango wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.









Dirisha dogo la usajili barani ulaya limefugwa hapo jana usiku huku ikimshuhudia winga raia wa Colombia Juan Cuadrado akitua kwa vinara wa soka wa ligi ya England Klabu ya Chelsea kwa dau la pauni milioni 23.3 kutoka timu ya Fiorentina ya Italia.
Huku wao Chelsea wakimuuza mshambuliaji wao Andre Schurrle kwenda Wolfsburg kwa Pauni Milioni 22, na kumtoa kwa mkopo winga Mohamed Salah kwa Fiorentina ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kumnunua Cuadrado.
Manchester United imefanya usajili wa kushangaza kwa kumsaini Beki wa Miaka 21, Andy Kellett,kwa mkopo toka Bolton Wanderers.





Jorge Mendes wakala wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo amesema mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 300 ikiwa ataamua kuihama klabu yake ya Real Madrid.
Wakala huyo amesema ikiwa timu yake itataka kuuza kwa sababu yoyote ile ni lazima timu inayomtaka itoe kiasi hicho cha fedha.
Ronaldo, mwenye wa miaka 29, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Dunia Mwezi uliopita alikua akihusishwa kurudi katika klabu yake zamani ya Manchester United.
Mendez akasisitiza kuwa nyota huyo atasalia katika timu ya Real Madrid pamoja na kupendwa na mashabiki wa Manchester United.

Wakala huyo aliyewahi kuwa Dj na mmiliki wa Klabu za usiku, ni mwakilishi wa nyota wengine katika soka kama Radamel Falcao, Angel Di Maria, James Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa. Pamoja na makocha Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari.




Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesema matokeo ya uchunguzi wa tuhuma za upangaji matokeo zinazowakabili waamuzi watatu wa Tanzania yatatolewa na shirikisho la dunia, FIFA baada ya uchunguzi kukamilika.




Kesho ni Ivorycoast dhidi ya Congo DRC AFCON 2015
Kikosi cha Ivory coast  kinachopigiwa upatu kutoroka na taji la kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu kitalazimika kuaga mashindano hayo wakati watakapokutana katika nusu fainali ya mashindano hayo kesho Jumatano dhidi ya Jamhuri ya Kemokrasia ya Kongo(Congo DRC).

Monday, February 2, 2015






Ivory Coast imeitwanga Algeria kwa mabao 3-1 katika mechi ya Kombe la Mataifa Afrika hatua ya robo fainali.

Mabao mawili ya Bony Wilfred aliyejiunga na Manchester City akitokea Swansea na moja la Gervinho yalitosha kuizima Algeria iliyoonyesha soka safi.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi, kwani pamoja na Tembo hao kuanza kufunga, lakini Algeria walisawazisha na kuwapa wakati mgumu Waafrika hao wa Magharibi.


Uwezo wa wachezaji mmojammoja kwa Ivory Coast pia ulichangia kuongeza uwezo wa kikosi hicho ambacho sasa kitakutana na DR Congo katika mechi ya nusu fainali.



Timu ya Taifa Ghana imekua timu ya tatu kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuibanjua Guinea kwa mabao 3-0.
Winga Christian Atsu ndie alienza kuipatia Ghana bao la kwanza dakika ya 4 ya mchezo kabla ya kuongeza tena bao la pili dakika ya 61.
Appiah akashindilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu lilifugwa dakika za lala salama za mchezo.
Guinea walipata pigo katika dakika za mwisho kwa kipa wao Naby Yattara kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea rafu mshambuliaji Asamoah Gyan.
Kwa ushindi huo Ghana au maarufu kwa jina la black Star watachuana na wenyeji Guinea ya Ikweta katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa katika dimba la Estadio De Malabo.