Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) liko mbioni kupata mdhamini wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Tunatarajia
mdhamini huyo atakuwa tayari kwa ajili ya msimu wa 2015/2016.
Ligi Daraja la Kwanza inashirikisha timu
24 zinazocheza katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kwa mtindo wa
nyumbani na ugenini.
Timu zinazocheza FDL msimu huu ni African
Lyon (Dar es Salaam), African Sports (Tanga), Ashanti United (Dar es Salaam),
Burkina Faso (Morogoro), Friends Rangers (Dar es Salaam), Geita Gold (Geita),
Green Warriors (Dar es Salaam), JKT Kanembwa (Kigoma), JKT Mlale (Ruvuma) na
JKT Oljoro (Arusha).
Nyingine ni Kimondo (Mbeya), Kinondoni
Municipal Council (Dar es Salaam), Kurugenzi (Iringa), Lipuli (Iringa),
Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Dar es
Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers (Tabora), Toto
Africans (Mwanza), na Villa Squad (Dar es Salaam).
wakati huohuo
Mechi za raundi
mbili za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi yote mawili
zimerudishwa nyuma kutokana na maombi ya klabu hizo kupungaza gharama za
kuendelea kuziweka kambini timu zao.
Hivyo,
Februari 8 mwaka huu kundi A litacheza mechi zake za raundi ya 21 wakati zile
za raundi 22 ambayo ndiyo ya mwisho zitafanyika Februari 13 mwaka huu. Mechi za
Februari 8 ni KMC vs African Lyon, Kurugenzi vs African Sports, Majimaji vs JKT
Mlale, Kimondo vs Friends Rangers, Ashanti United vs Villa Squad, Polisi Dar vs
Lipuli.
Februari
13 mwaka huu ni African Lyon vs Polisi Dar, Kurugenzi vs Lipuli, Kimondo vs
Majimaji, JKT Mlale vs Ashanti United, Friends Rangers vs African Sports, na
Villa Squad vs KMC.
Kwa
upande wa kundi B wataanza mechi za raundi 22 Februari 10 mwaka huu ili kupisha
mechi za viporo za Polisi Mara zinazomalizika Februari 5 mwaka huu. Hivyo,
Februari 10 mwaka huu itakuwa ni Burkina Faso vs JKT Kanembwa, Mwadui vs Polisi
Tabora, Polisi Dodoma vs Green Warriors, Rhino Rangers vs JKT Oljoro, Panone vs
Polisi Mara, Geita Gold vs Toto Africans.
No comments:
Post a Comment