Monday, February 2, 2015






Ivory Coast imeitwanga Algeria kwa mabao 3-1 katika mechi ya Kombe la Mataifa Afrika hatua ya robo fainali.

Mabao mawili ya Bony Wilfred aliyejiunga na Manchester City akitokea Swansea na moja la Gervinho yalitosha kuizima Algeria iliyoonyesha soka safi.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi, kwani pamoja na Tembo hao kuanza kufunga, lakini Algeria walisawazisha na kuwapa wakati mgumu Waafrika hao wa Magharibi.


Uwezo wa wachezaji mmojammoja kwa Ivory Coast pia ulichangia kuongeza uwezo wa kikosi hicho ambacho sasa kitakutana na DR Congo katika mechi ya nusu fainali.



Timu ya Taifa Ghana imekua timu ya tatu kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuibanjua Guinea kwa mabao 3-0.
Winga Christian Atsu ndie alienza kuipatia Ghana bao la kwanza dakika ya 4 ya mchezo kabla ya kuongeza tena bao la pili dakika ya 61.
Appiah akashindilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu lilifugwa dakika za lala salama za mchezo.
Guinea walipata pigo katika dakika za mwisho kwa kipa wao Naby Yattara kupewa kadi nyekundi kwa kumchezea rafu mshambuliaji Asamoah Gyan.
Kwa ushindi huo Ghana au maarufu kwa jina la black Star watachuana na wenyeji Guinea ya Ikweta katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa katika dimba la Estadio De Malabo.


No comments:

Post a Comment