Kipa bora wa michuano ya Kombe la Taifa la
Wanawake, Belina Julius wa Temeke amezawadiwa sh. 500,000 na Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.
Dk
Mukangara alitoa zawadi hiyo baada ya mechi ya fainali ya michuano
iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es
Salaam. Dk Mukangara alikuwa mgeni rasmi kwenye fainali hiyo.
Temeke ndiyo walioibuka mabingwa wa
michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini baada ya kuilaza Pwani bao
1-0 katika fainali iliyoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni ya Azam.
Ilala ilifanikiwa kutwaa baada ya kuichapa
Kigoma mabao 3-0. Bingwa amepata sh. milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni
mbili wakati mshindi wa tatu ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo
iliyodhaminiwa na kampuni ya Proin.
No comments:
Post a Comment