Dirisha dogo la usajili barani ulaya limefugwa
hapo jana usiku huku ikimshuhudia winga raia wa Colombia Juan Cuadrado akitua
kwa vinara wa soka wa ligi ya England Klabu ya Chelsea kwa dau la pauni milioni
23.3 kutoka timu ya Fiorentina ya Italia.
Huku wao Chelsea wakimuuza mshambuliaji wao Andre Schurrle kwenda Wolfsburg
kwa Pauni Milioni 22, na kumtoa kwa mkopo winga Mohamed Salah kwa Fiorentina
ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kumnunua Cuadrado.
Manchester United imefanya usajili wa kushangaza kwa kumsaini Beki wa Miaka
21, Andy Kellett,kwa mkopo toka Bolton Wanderers.
No comments:
Post a Comment