Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), John
Ambwene Mwakalobo uliotokea jana (Februari 1 mwaka huu) mkoani Iringa baada ya
kuanguka akiwa nyumbani kwake.
Msiba
huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa mpira wa miguu kwani wakati wa uhai wake,
Mwakalobo alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti wa IRFA, kabla ya 2012 kushinda nafasi ya Katibu Msaidizi.
Alizaliwa
Februari 4, 1954 na kupata elimu ya sekondari katika shule ya Azania, Dar es
Salaam na baadaye mafunzo ya ualimu kwenye Chuo cha Ualimu Mpwapwa mkoani
Dodoma. Alianzia kazi ya ualimu Newala mkoani Mtwara kabla ya kuhamia mkoani
Iringa mwaka 1981. Alistaafu mwaka 2013.
TFF
inatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu kwa msiba huo.
Marehemu
anatarajiwa kuzikwa kesho (Februari 3 mwaka huu) kwao Kyela mkoani Mbeya.
Ameacha mke, watoto wanne na mjukuu mmoja. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina
lake lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment