Kikosi cha Ivory coast kinachopigiwa upatu kutoroka na taji la kombe
la mataifa ya Afrika mwaka huu kitalazimika kuaga mashindano hayo wakati watakapokutana
katika nusu fainali ya mashindano hayo kesho Jumatano dhidi ya Jamhuri ya
Kemokrasia ya Kongo(Congo DRC).
Pambano hilo la kesho Jumatano(04.02.2015)
litafanyika Estadio de Bata saa nne(22:00) kamili usiku kati ya timu hiyo iliyoshiriki
katika fainali za kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil na Congo DRC, ni mchezo unaoangaliwa kwa karibu na wadadisi
na wapenzi wa michezo barani Afrika miongoni mwa timu nne zilizofanikiwa
kuingia katika nusu fainali wakati michuano hiyo ya wiki tatu ikiingia katika
awamu ya kuelekea fainali.
Algeria , timu inayoongoza katika
orodha ya FIFA kwa timu za Afrika , ilionyesha mafanikio katika miezi 12
iliyopita, ikiwa ni pamoja na kuilazimisha Ujerumani ambayo ni mabingwa wa
dunia kuingia katika muda wa nyongeza katika mchezo wao wa kombe la dunia
nchini Brazil.
Tangu wakati huo ushindi mara tano
katika michezo sita katika michezo ya kufuzu kuingia katika fainali za kombe la
Afrika imefuatiwa na ushindi katika awamu ya makundi dhidi ya Afrika kusini na
Senegal.
Mshambuliaji huyo mpya wa Manchester City aliifungia timu yake bao la kwanza
kwa kichwa kufuatia krosi iliyochongwa na Max Gradel katika dakika ya 26 ya
mchezo.Hilal Soudani aliisawazishia Algeria katika dakika ya 51 na baadaye kumlazimisha mlinda mlango wa Ivory Coast, Sylvain Gbohouo kuokoa mpira uliokuwa unaelekea wavuni.
Kazi nzuri ya Gbohouo ilijibiwa na bao la pili la Bony ambaye alitumia vema mpira wa adhabu uliopigwa na Yaya Toure kufunga tena kwa kichwa. Gervinho alihitimisha kichapo cha Ivory Coast kwa Algeria pale alipofunga goli la tatu katika dakika ya 90 na kuzima kabisa ndoto za Algeria kucheza nusu fainali za michuano hiyo.
Congo DRC walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kuwanyuka Jirani zao Congo Brazaville Bao 4-2 huko Estadio de Bata Mjini Bata Nchini Equatorial Guinea na kutinga Nusu Fainali.
Congo walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 55 baada ya Frikiki ya Ndinga kuunganishwa na Férébory Dore.
Bao la Pili la Congo lilifungwa Dakika ya 62 kupitia Thievy Bifoum kufuatia makosa ya Kasusula na kumfanya Kipa Kidiaba aokoe Mpira toka kwa Dore lakini ukamrudia Thievy Bifoum aliefunga na kuifanya Gemu iwe Congo 2 Congo DR 0.
Congo DRC wakafufuka na kupiga Bao 4 kupitia Mbokani, Dakika ya 65, Loteteka Bokila, Dakika ya 75, Joel Kimwaki, Dakika ya 81, na Mbokani tena Dakika ya 90 na kusonga Nusu Fainali.
Kikosi cha Ivory Coast kinatarajiwa kuwa hivi: Gbohouo; Bailly, K. Toure, Kanon; Aurier, Y. Toure, Die, Tiene; Gervinho, Bony, Gradel.
Akiba: Barry, Sayouba, Viera, Doukoure, Akpa-Akpro, Diomande, Assale, Doumbia, Kalou, Tallo, Traore.
Wakati Congo DRC: Kidiaba, Issama, Mongongu, Zakuani, Kasusula, Mabwati, Makiadi, Mbemba, Bokila, Mbokani, Bolasie
Akiba: Oualembo, Munganga, Mulumbu, Kage, Kebano, Mabele, Kabananga, Kimwaki, Kudimbana, Mabidi, Mubele, Mandanda
Mechi za mwisho zitachezwa Jumamosi Februari 7, 2015 huko Nuevo Estadio de Malabo wenye uwezo wa kubeba watazamaji 15,250 mjini Malabo nchini Equatorial Ginea kutafuta mshindi wa tatu, huku fainali ikitarajiwa kuchezwa Jumapili Februari 8,2014 huko Estadio de Bata wenye uwezo wa kumudu watazamaji 37,500 mjini Bata nchini Guinea mechi zote zitachezwa majira ya saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.
Droo ya Kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Barani Afrika{ Afcon 2015} ilifanyika huko Cairo nchini Misri huku timu zote za kanda ya Afrika Mashariki zikiratibiwa kucheza katika mechi za mchujo kuanzia mwezi Mei, 2014 hadi Juni, 2014 kabla ya kushiriki mechi za kufuzu.
Kenya ikachuana dhidi ya Visiwa vya Comoro ,Tanzania ikapambana na Zimbabwe, Uganda ikatoana kijasho dhidi ya Madagascar nayo Rwanda ikivaana na Libya.
Burundi kwa upande wake ikachuana dhidi ya Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiratibiwa kuvaana na Namibia.
Baada ya kushiriki mkondo wa kwanza wa maondoano mataifa hayo tena yakalazimika kuchuana miongoni mwao ilikufuzu kwa awamu ya pili.
Katika mechi zilizoibua hisia ni pamoja na mabingwa watetezi Nigeria ambao waliratibiwa kuvaana na Afrika Kusini mechi zilizoanza septemba hadi Novemba 2014 na kumalizika kwa Nigeria kutupwa nje ya michuano hiyo.
Mahasimu wa jadi kaskazini mwa Afrika Tunisia na Misri waliratibiwa kukwaruzana nayo Ghana,ikitoana kijasho na Togo.Aidha Ivory Coast ikafungua kampeni yake ya kufuzu dhidi ya mahasimu wao wakuu Cameroon.
Washindi wawili katika kila kundi walitarajiwa kujiunga na wenyeji Morocco kwenye kipute cha kuwania taji la ubingwa barani Afrika 2015, hata hivyo kufuatia hofu ya ugonjwa wa Ebola Morroco walijitoa katika uenyeji huo hivyo nafasi yao kuchukuliwa na Guinea ya Ikweta ambao pia waliwashinda nchi ya Tanzania ambao walitaka kuchangamkia fursa ya uenyeji huo.
Guinea wakawa wenyeji wa michuano hii baada ya Morroco waliokuwa wenyeji kujitoa kwa hofu ya maambukizi ya ugojwa wa ebola.
Mataifa 16 ya Afrika yakashiriki michuano hiyo ambapo iligawanywa katika makundi manne.
Kundi A linaongozwa na wenyeji Guinea ya Ikweta ,Burkina Faso ,Gabon na Congo.
Kundi B Zambia,Tunisia,Cape Verde na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Kundi C Ghana Algeria Afrika Kusini Senegal.
Kundi D Ivory Coasty Mali Cameroon Guinea.
Viwanja vilikavyotumika katika michuano ni Nuevo Estadio de Malabo, ulioko mji mkuu wa Malabo, wenye uwezo wa kuchukua Watazamaji 15,250 na uwanja mwingine ni Estadio de Bata, ulioko mjini Bata, wenye kuchukua Watazamaji 37,500.
Viwanja vingine ni-Estadio de Mongomo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000, na Nuevo Estadio de Ebebiyín unaomudu watazamaji Watazamaji 5,000
Jumla ya waamuzi 44 waliteuliwa kuchezesha michuano hiyo.
Kundi D ndio lililooneka kama kundi la kifo kwa kuwepo vigogo Cameroon na Ivory Coast huku vigogo hao wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa uchampion wa michuano hiyo.
Timu nyingine zinazopigiwa upatu wa kutwaa kombe hilo ni Ghana, Afrika kusini Senegal pamoja na Zambia kutoka na ubora wa vikosi vyao.
Nyota waliotarajiwa kutamba katika michuano hii ni pamoja na kiungo Yaya Toure, mshambuliaji Emmanuel Mayuka wa Zambia Papiss Demba Cisse, Eric Choupo-Moting Gervinho. Bernard Parker wa afrika kusini Asamoah Gyan wa Ghana na mshambuliajin Pierre-Emerick Aubameyang
Kukosekana kwa Timu vigogo kama Nigeria ,Misri pamoja na Angola na majina ya wachezaji wakubwa kama Didie Drobga, John mikel obi na Mohamed Aboutrika kulionekana kama kunaweza kupunguza mvuto wa michuano hiyo.
Libya walitwaa uchampion wa wa Afrika katika michuano iliyopita swali ni nani ataibuka bigwa kwa Mwaka huu?
No comments:
Post a Comment