Mkuu wa kitengo cha polisi jamii, Ntogwa Bundala
POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA
waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama
hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya
wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya
Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo
katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe
uliokusudiwa.
Katika
purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na
wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14
wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Aidha Polisi
walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na
silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo
likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka
waandamanaji.
Licha ya
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado
halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.