Friday, September 26, 2014

MAANDAMANO CHADEMA


  Mkuu wa kitengo cha polisi jamii, Ntogwa Bundala
POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Katika purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Aidha Polisi walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka waandamanaji. 
Licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.

No comments:

Post a Comment