Mwanasiasa huyo kutoka chama cha PAN amembagua
Ronaldinho akimfananisha na sokwe.
Sababu kubwa ya kumbagua ni kutokana na foleni kubwa
ya magari barabarani iliyosababishwa na mashabiki wa timu ua Querétaro
aliyojiunga nayo nchini Mexico.
Wengi walikuwa wanatokea uwanjani wakati Ronaldinho
anatambulishwa.
Mwanasiasa huyo akaamua kuandika kwenye ukurasa wake
wa Facebook, kama anachukizwa na mchezo wa soka na anashangazwa watu
kusababisha foleni sababu ya sokwe mmoja.
Kauli hiyo ilipingwa na wengi na kusababisha
mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri kuifuta post yake.
Hata hivyo, watu wameendelea kumsakama na kupinga
kitendo chake hicho cha kibaguzi.
No comments:
Post a Comment