Ngassa amesema kuwa Azam walionyesha kiwango kikubwa
kipindi cha kwanza na Yanga walicheza kawaida sana.
Aliongeza kuwa, tatizo lililosababisha wasifunge
mabao kipindi cha kwanza ilitokana na mshambuliaji wao, Mbrazili, Geilson
Santana ‘Jaja’ kutotokea mapema kwenye boksi kwa ajili ya kuunganisha krosi.
“Inaniuma kwa kuwa sijafunga bao lolote licha ya
kupata nafasi nyingi lakini ilinitokea kwa bahati mbaya.”
Katika mechi hiyo, Yanga ilibanwa sana katika
kipindi cha kwanza, lakini Azam FC wakashindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
katika kipindi cha pili, ngoma ikabadilika na Yanga
kutawala huku wakifanikiwa kupata mabao matatu yaliyoinyamazisha Azam FC.
Ngassa alijiunga na Yanga SC mwaka 2007 na kabla hajahamia
Azam FC alishinda mataji matatu Jangwani, ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili na
Kombe la Tusker mara moja.
MATAJI ALIYOWAHI KUSHINDA MRISHO NGASSA
2006 Tusker Kagera Sugar
2008 Ligi Kuu Yanga SC
2009 Ligi Kuu Yanga SC
2009 Tusker Yanga SC
2010 Challenge Kili Stars
2011 Mapinduzi Azam FC
2012: Ngao
Simba SC
2013 Ngao Yanga SC
2014 Ngao Yanga SC
Wakati anaingia Yanga SC Ngassa alikuwa ameshinda taji moja
tu, Kombe la Tusker akiwa na Kagera Sugar.
Na alipokwenda Azam FC mwaka 2010, Ngassa pamoja na
kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, pia alishinda Kombe la Mapinduzi na
klabu hiyo.
Alipohamia Simba SC nako akashinda Ngao ya Jamii katika
msimu mmoja wa kuitumikia na baada ya kurejea Yanga SC, ametwaa Ngao mara mbili
mfululizo.
Hata hivyo, mwaka jana Ngassa alijiunga na wenzake
kusherehekea ushindi wa Ngao kwa kuifunga Azam tena 1-0 akitokea jukwaani, kwa
sababu alikuwa anatumikia adhabu.
Ngassa ambaye kwa sasa anaongoza kwa mabao katika Ligi ya
Mabingwa Afrika, ingawa Yanga ilikwishatolewa mapema, pia amewahi kushinda
Kombe la Challenge akiwa na Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
No comments:
Post a Comment