MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck jana
alikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa
hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund, lakini
akashindwa kuitumia.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16
kutoka kwa wapinzani, Manchester United jana alienedelea kupewa nafasi katika
kikosi cha kwanza cha The Gunners na kocha Arsene Wenger akionyesha alimsajili
kwa sababu alimuamini, lakini akashindwa kuwafurahisha mashabiki.
Muingereza huyo jana alipata nafasi tatu nzuri za
kuifungia Arsenal mabao kuanzia mapema kipindi cha kwanza, lakini zote
akashindwa kuzitumia, The Gunners wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund ugenini.
No comments:
Post a Comment