Mabingwa wa kombe la dunia 2014 kwa watoto wa
mitaani nchini, timu ya Tanzania Street Childrens (TSC) wameanza ziara ya
kusaka vipaji kwaajili ya kombe la dunia lijalo, baada ya kufanikiwa kutwaa
kombe hilo mwaka huu nchini Brazil.
TSC wameanza kusaka vipaji hivyo kupitia programme
ya Street Skills na School Programme ambazo zinahusisha watoto wanaoishi katika
mitaa hususani katika maeneo ya Ilemela, Mjini kati na Mabatini.
Akizungumza na gazeti hili, katibu wa TSC Daniel Yangwe
amebainisha kuwa, maandalizi haya ni sehemu ya kuhakikisha wanalitetea taji lao
msimu ujao wa kombe la dunia.
“Lengo la Programme hizi zinalenga kuwaelimisha
watoto kupitia soka kuwa kuishi katika mitaa kunachangia wao kuendelea kuwa
maskini, lakini pia kupata vipaji ambavyo vitasaidia kupata timu itakayoshiriki
katika michezo ya kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika kombe la dunia msimu
ujao”alisema Yangwe.
“Tumefanikiwa kupata watoto kumi ambao wanavipaji na
tayari wameingia katika timu yetu ila bado tunaendelea kusaka vipaji ili wale
ambao watapata elimu ya kutosha waweze kurejea makwao na wengine wakae kambini
kwetu ambao hawana kabisa familia”alisongeza.
Programme hizi zina makocha wawili kila moja, huku
zikijumuisha maeneo ya Kirumba katika uwanja wa Furahisha kwa wale wenye umri
chini ya miaka 15 na miaka chini ya 18, Mjinin kati wanatumia uwanja wa
Nyamagana kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 na chini ya miaka 12, huku
kwa upande wa shule wakitumia shule za Sabasaba, Mwenge, Kitangiri na Igoma.
No comments:
Post a Comment