RONALDO APIGA NNE REAL
NYOTA Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick yake ya 25 akiwa
na Real Madrid kikosi cha Carlo Ancelotti kikifikisha mabao 18 katika mechi
tatu kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Elche katika La Liga.
Ronaldo alifikisha mabao nane ndani ya wiki na baada ya
mechi alipoulizwa kama bado ana furaha Madrid alisema."Mambo yanakwenda
vizuri na zaidi binafasi na timu inafunga mabao, inashinda mechi na kucheza
vizuri.’
Alipoulizwa kuhusu kauli ya karibuni ya Jose Mourinho kwamba
wawili hao kwa sasa hawana uhusiano tena, "Si juu yangu kuzungumza mambo
kama hayo, nafikiria juu ya kile tunachokifanya uwanjani," amesema.
Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Albacar
Gallego kwa penalti ya utata iliyotolewa na refa Carlos Gomez, lakini Gareth
Bale akasawazisha akimalizia krosi ya James Rodriguez kabla ya Cristiano
Ronaldo kufunga mabao manne, mawili ya penalti na kufikisha hat-trick 25 akiwa
na Los Blancos.
No comments:
Post a Comment