Friday, November 21, 2014

USO KWA USO MAN U VS ARSENAL





Uso kwa Uso
Arsenal v Man United

RONALDO KUMEKUCHA


Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.

GERNINHO AKIONA CHA MOTO

                               

Askari waliokua wanatekeleza jukumu la kuangalia usalama katika uwanja wa FĂ©lix HouphouÄ—t-Boigny, huko mjini Abidjan ambao ulitumika kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kundi la nne kati ya timu ya taifa ya Ivory Coast dhidi ya Cameroon walilazimika kutumia nguvu baada ya mashabiki kuingia katika sehemu ya kucheza mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na muamuzi Bouchaļb El Ahrach kutoka nchini Morocco.

NIGERIA NJE AFCON 2015

                                       
                                       
                                          

Mabingwa wa soka barani Afrika timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles wameshindwa kufuzu kucheza fainali za mwaka 2015 ambazo zimepangwa kufanyika Equatorial Guinea badala ya Morocco walioamua kuipiga teke nafasi ya kuwa mwenyeji.

KUTOKAMILIKA VIWANJA VYA AALIANCE KUCHANGIA KUONGEZWA MUDA



Michuano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 inayoshirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30 mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.

DARAJA LA PILI KUANZA DESEMBA 2

Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa kushuhudia michezo kumi katika viwanja vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.

MAKOCHA WANOLEWA


Friday, September 26, 2014

MAANDAMANO CHADEMA


  Mkuu wa kitengo cha polisi jamii, Ntogwa Bundala
POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
Katika purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Aidha Polisi walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka waandamanaji. 
Licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.

MAANDAMANO CHADEMA

POLISI mkoani Mwanza wamewatia mbaroni viongozi sita na wafuasi kadhaa wa CHADEMA waliokuwa wakijiandaa kuandamana ikiwa ni hatua mara baada ya wanachama hao kukaidi amri ya polisi iliyowekwa ya kusitisha maandamano. Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5.20 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kuanza maandamano yaliyokuwa yaanzie Viwanja vya Sahara mkoni Mwanza hadi Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana zilizopo katikati ya na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Katika purukushani hiyo iliyodumu zaidi ya masaa mawili huku ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu, Polisi wamewatia mbaroni watu takribani 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali. Aidha Polisi walionekana kutanda kwenye maeneo mbalimbali jijini hapa wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku gari la maji ya kuwasha nalo likipita mitaa kadhaa ya barabara muhimu kuashiria kuwasaka waandamanaji. Licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili na idadi ya watu inayowashikilia.

Wednesday, September 17, 2014

NGASSA BADO NYOTA INA NG'AA


MAKALI YA DANNY WELBECK BADO



MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck jana alikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund, lakini akashindwa kuitumia.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka kwa wapinzani, Manchester United jana alienedelea kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha The Gunners na kocha Arsene Wenger akionyesha alimsajili kwa sababu alimuamini, lakini akashindwa kuwafurahisha mashabiki.



 Muingereza huyo jana alipata nafasi tatu nzuri za kuifungia Arsenal mabao kuanzia mapema kipindi cha kwanza, lakini zote akashindwa kuzitumia, The Gunners wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund ugenini. 

UBAGUZI WA RANGI WAENDELEA KURINDIMA


Mwanasiasa huyo kutoka chama cha PAN amembagua Ronaldinho akimfananisha na sokwe.
Sababu kubwa ya kumbagua ni kutokana na foleni kubwa ya magari barabarani iliyosababishwa na mashabiki wa timu ua Querétaro aliyojiunga nayo nchini Mexico.
Wengi walikuwa wanatokea uwanjani wakati Ronaldinho anatambulishwa.
Mwanasiasa huyo akaamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, kama anachukizwa na mchezo wa soka na anashangazwa watu kusababisha foleni sababu ya sokwe mmoja.
Kauli hiyo ilipingwa na wengi na kusababisha mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri kuifuta post yake.
Hata hivyo, watu wameendelea kumsakama na kupinga kitendo chake hicho cha kibaguzi.